2 Chronicles 5:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walawi wote waimbaji, wakiwamo Asafu, Hemani, na Yeduthuni, pamoja na Walawi wengine wa koo zao, wakiwa wamejivalia nguo zao za kitani safi huku wamebeba matoazi, vinanda na vinubi, walisimama upande wa mashariki wa madhabahu. Makuhani 120 wapiga tarumbeta walikuwa pamoja nao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walawi wote waliokuwa waimbaji, yaani Asafu, Hemani, Yeduthuni, wana wa ndugu zao, walisimama upande wa mashariki wa madhabahu, wakiwa wamevaa kitani safi huku wakipiga matoazi, vinubi na zeze. Walikuwa pamoja na makuhani mia moja na ishirini wakipiga tarumbeta.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
tena Walawi waimbaji, wote pia, yaani Asafu, na Hemani, na Yeduthuni, na wana wao, na ndugu zao, hali wamevaa kitani safi, wenye matoazi na vinanda na vinubi, wamesimama upande wa mashariki wa madhabahu, na pamoja nao makuhani mia na ishirini wakipiga panda;)
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walawi wote waimbaji, wakiwamo Asafu, Hemani, na Yeduthuni, pamoja na Walawi wengine wa koo zao, wakiwa wamejivalia nguo zao za kitani safi huku wamebeba matoazi, vinanda na vinubi, walisimama upande wa mashariki wa madhabahu. Makuhani 120 wapiga tarumbeta walikuwa pamoja nao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walawi wote waliokuwa waimbaji, yaani, Asafu, Hemani, Yeduthuni, wana wa ndugu zao, walisimama upande wa mashariki wa madhabahu, wakiwa wamevaa kitani safi huku wakipiga matoazi, vinubi na zeze. Walikuwa pamoja na makuhani 120 wakipiga tarumbeta.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walawi wote waliokuwa waimbaji, yaani, Asafu, Hemani, Yeduthuni, wana wa ndugu zao, walisimama upande wa mashariki wa madhabahu, wakiwa wamevaa kitani safi huku wakipiga matoazi, vinubi na zeze. Walikuwa pamoja na makuhani 120 wakipiga tarumbeta.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
tena Walawi waimbaji, wote pia, yaani Asafu, na Hemani, na Yeduthuni, na wana wao, na ndugu zao, wakiwa wamevaa kitani safi, wenye matoazi na vinanda na vinubi, wamesimama upande wa mashariki wa madhabahu, na pamoja nao makuhani mia moja na ishirini wakipiga panda;)
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walawi wote waimbaji, wakiwamo Asafu, Hemani, na Yeduthuni, pamoja na Walawi wengine wa koo zao, wakiwa wamejivalia nguo zao za kitani safi huku wamebeba matoazi, vinanda na vinubi, walisimama upande wa mashariki wa madhabahu. Makuhani 120 wapiga tarumbeta walikuwa pamoja nao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
nao waimbaji wote pia walio Walawi, wale wa Asafu na wa Hemani na wa Yedutuni pamoja na wana wao na ndugu zao, wote walikuwa wamevaa nguo za bafta, wakashika patu na mapango na mazeze, wakawa wamesimama upande wa maawioni kwa jua penye meza ya kutambikia, tena walikuwako pamoja na watambikaji 120 wenye kupiga matarumbeta.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
tena Walawi waimbaji, wote pia, yaani Asafu, na Hemani, na Yeduthuni, na wana wao, na ndugu zao, hali wamevaa kitani safi, wenye matoazi na vinanda na vinubi, wamesimama upande wa mashariki wa madhabahu, na pamoja nao makuhani mia na ishirini wakipiga panda;)
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walawi wote waimbaji, pamoja na Asafu, Hemani, na Yedutuni, pamoja na Walawi wengine wa ukoo zao, wakiwa wamevaa nguo zao za kitani safi nao wakabeba matoazi, vinanda na vinubi, walisimama upande wa mashariki wa mazabahu. Makuhani mia moja na makumi mbili wapiga baragumu walikuwa pamoja nao.