2 Chronicles 5:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha makuhani wakaliingiza sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu mahali pake, katika chumba cha ndani cha nyumba, mahali patakatifu sana, chini ya mabawa ya wale viumbe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Makuhani wakalileta Sanduku la Agano la Mwenyezi Mungu hadi mahali patakatifu ndani ya Hekalu, pale Patakatifu pa Patakatifu, na kuliweka chini ya mabawa ya makerubi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Makuhani wakaliingiza sanduku la agano la Bwana mahali pake katika chumba cha ndani cha nyumba, patakatifu pa patakatifu, yaani, chini ya mabawa ya makerubi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha makuhani wakaliingiza sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu mahali pake, katika chumba cha ndani cha nyumba, mahali patakatifu sana, chini ya mabawa ya wale viumbe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha makuhani wakaleta Sanduku la Agano la BWANA mpaka mahali pake ndani ya mahali Patakatifu pa Hekalu, yaani, mahali Patakatifu pa Patakatifu na kuliweka chini ya mabawa ya wale makerubi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Makuhani wakalileta Sanduku la Agano la bwana hadi mahali pake ndani ya sehemu takatifu ndani ya Hekalu, yaani Patakatifu pa Patakatifu, na kuliweka chini ya mabawa ya makerubi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Makuhani wakaliingiza sanduku la Agano la BWANA mahali pake katika chumba cha ndani cha nyumba, patakatifu pa patakatifu, yaani, chini ya mabawa ya makerubi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha makuhani wakaliingiza sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu mahali pake, katika chumba cha ndani cha nyumba, mahali patakatifu sana, chini ya mabawa ya wale viumbe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watambikaji wakaliingiza Sanduku la Agano la Bwana mahali pake katika chumba cha ndani kiitwacho Patakatifu Penyewe, wakaliweka chini ya mabawa ya Makerubi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Makuhani wakaliingiza sanduku la agano la BWANA mahali pake katika chumba cha ndani cha nyumba, patakatifu pa patakatifu, yaani, chini ya mabawa ya makerubi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha makuhani wakaingiza Sanduku la Agano la Yawe pahali pake, katika chumba cha ndani cha nyumba, Pahali Patakatifu Sana, chini ya mabawa ya makerubi.