2 Chronicles 5:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa kuwa mipiko hiyo ilikuwa mirefu sana, ncha zake ziliweza kuonekana kutoka mahali patakatifu mbele ya chumba cha ndani, lakini haikuweza kuonekana kutoka upande wa nje. Mipiko hiyo ingali mahali hapo hata leo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mipiko hiyo ilikuwa mirefu sana kiasi kwamba ncha zake zilizojitokeza kutoka Sanduku, nazo zilionekana ukiwa mbele ya Patakatifu pa Patakatifu, lakini sio nje ya Mahali Patakatifu. Hiyo mipiko ipo hata leo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na ile miti ilikuwa mirefu, hata ncha za miti zilionekana sandukuni mbele ya chumba cha ndani, lakini hazikuonekana nje; nayo iko kuko huko hata leo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa kuwa mipiko hiyo ilikuwa mirefu sana, ncha zake ziliweza kuonekana kutoka mahali patakatifu mbele ya chumba cha ndani, lakini haikuweza kuonekana kutoka upande wa nje. Mipiko hiyo ingali mahali hapo hata leo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mipiko hiyo ilikuwa mirefu sana kiasi kwamba ncha zake zilizojitokeza kutoka kwenye Sanduku, nazo zingeweza kuonekana ukiwa ndani mbele ya mahali Patakatifu, lakini siyo ukiwa nje ya mahali patakatifu, nayo hiyo mipiko ipo mpaka leo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mipiko hiyo ilikuwa mirefu sana kiasi kwamba ncha zake zilizojitokeza kutoka kwenye Sanduku, nazo zilionekana ukiwa mbele ya Patakatifu pa Patakatifu, lakini sio nje ya Mahali Patakatifu. Hiyo mipiko ipo hata leo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na ile miti ilikuwa mirefu, hata ncha za miti zilionekana sandukuni mbele ya chumba cha ndani, lakini hazikuonekana nje; nayo iko huko huko hata leo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa kuwa mipiko hiyo ilikuwa mirefu sana, ncha zake ziliweza kuonekana kutoka mahali patakatifu mbele ya chumba cha ndani, lakini haikuweza kuonekana kutoka upande wa nje. Mipiko hiyo ingali mahali hapo hata leo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa urefu wa mipiko pembe zao hii mipiko zikaoneka kutoka penye Sanduku kuelekea mle chumbani mwa ndani, lakini nje hazikuoneka; nayo imo humo mpaka siku hii ya leo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na ile miti ilikuwa mirefu, hata ncha za miti zilionekana sandukuni mbele ya chumba cha ndani, lakini hazikuonekana nje; nayo iko kuko huko hata leo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa sababu miti ile ilikuwa mirefu sana, incha zake ziliweza kuonekana kutoka Pahali Patakatifu mbele ya chumba cha ndani, lakini haikuweza kuonekana kutoka upande wa inje. Miti ile ingali pahali pale hata leo.