2 Chronicles 6:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Solomoni alikuwa ametengeneza jukwaa la shaba ambalo aliliweka katikati ya ua. Urefu na upana wake ulikuwa mita mbili na robo, na kimo chake mita moja na robo. Alipanda jukwaani na kupiga magoti mbele ya jumuiya yote ya Israeli, akainua mikono yake kuelekea mbinguni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Sulemani alikuwa ametengeneza jukwaa la shaba, urefu wake dhiraa tano, na upana wake dhiraa tano na kimo chake dhiraa tatu, naye akaliweka katikati ya ukumbi wa nje. Akapanda juu ya hilo jukwaa kisha akapiga magoti mbele ya kusanyiko lote la Israeli, akanyoosha mikono yake kuelekea mbinguni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
(maana Sulemani alikuwa amefanya mimbari ya shaba, urefu wake mikono mitano, na upana wake mikono mitano, na kwenda juu kwake mikono mitatu, na kuisimamisha katikati ya ua; akasimama juu yake, akapiga magoti mbele ya mkutano wote wa Israeli, akaikunjua mikono yake kuelekea mbinguni);
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Solomoni alikuwa ametengeneza jukwaa la shaba ambalo aliliweka katikati ya ua. Urefu na upana wake ulikuwa mita mbili na robo, na kimo chake mita moja na robo. Alipanda jukwaani na kupiga magoti mbele ya jumuiya yote ya Israeli, akainua mikono yake kuelekea mbinguni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi alikuwa ametengeneza jukwaa la shaba, urefu wake dhiraa tano, na upana wake dhiraa tano na kimo chake dhiraa tatu, naye akaliweka katikati ya ukumbi wa nje. Akapanda juu ya hilo jukwaa kisha akapiga magoti mbele ya kushanyiko lote la Israeli, akanyosha mikono yake kwelekea mbinguni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Sulemani alikuwa ametengeneza jukwaa la shaba, urefu wake dhiraa tano, na upana wake dhiraa tano na kimo chake dhiraa tatu, naye akaliweka katikati ya ukumbi wa nje. Akapanda juu ya hilo jukwaa kisha akapiga magoti mbele ya kusanyiko lote la Israeli, akanyoosha mikono yake kwelekea mbinguni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
(maana Sulemani alikuwa amefanya mimbari ya shaba, urefu wake dhiraa tano, na upana wake dhiraa tano, na kwenda juu kwake dhiraa tatu, na kuisimamisha katikati ya ua; akasimama juu yake, akapiga magoti mbele ya mkutano wote wa Israeli, akaikunjua mikono yake kuelekea mbinguni);
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Solomoni alikuwa ametengeneza jukwaa la shaba ambalo aliliweka katikati ya ua. Urefu na upana wake ulikuwa mita mbili na robo, na kimo chake mita moja na robo. Alipanda jukwaani na kupiga magoti mbele ya jumuiya yote ya Israeli, akainua mikono yake kuelekea mbinguni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani Salomo alikuwa ametengeneza hapo ulingo wa shaba, akauweka hapo uani katikati, urefu wake ulikuwa mikono mitano, nao upana wake mikono mitano, nao urefu wake wa kwenda juu ulikuwa mikono mitatu, akasimama hapo juu, akayapiga magoti yake machoni pao mkutano wote wa Waisiraeli, akaikunjua mikono yake na kuielekeza mbinguni,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
(maana Sulemani alikuwa amefanya mimbari ya shaba, urefu wake mikono mitano, na upana wake mikono mitano, na kwenda juu kwake mikono mitatu, na kuisimamisha katikati ya ua; akasimama juu yake, akapiga magoti mbele ya mkutano wote wa Israeli, akaikunjua mikono yake kuelekea mbinguni);
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Solomono alikuwa ametengeneza mimbari ya shaba ambayo aliweka katikati ya kiwanja. Urefu na upana wake ulikuwa metre mbili na sentimetre makumi mbili na tano, na urefu kwenda juu metre moja na sentimetre makumi mbili na tano. Akapanda juu ya mimbari na kupiga magoti mbele ya watu wote wa Israeli, akainua mikono yake kuelekea mbinguni.