2 Chronicles 6:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Aliomba akisema, “Ee, Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu mwingine kama wewe, mbinguni ama duniani. Wewe ni mwaminifu, kwani umetimiza agano lako na kuwaonesha fadhili zako watumishi wako wanaoishi wakikutii kwa moyo wao wote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akasema: “Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe juu mbinguni wala chini duniani, wewe unayetunza agano lako la upendo na watumishi wanaodumu katika njia yako kwa moyo wote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akasema, Ee Bwana, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe, mbinguni, wala duniani; ushikaye maagano na rehema kwa watumishi wako, waendao mbele zako kwa moyo wao wote;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Aliomba akisema, “Ee, Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu mwingine kama wewe, mbinguni ama duniani. Wewe ni mwaminifu, kwani umetimiza agano lako na kuwaonesha fadhili zako watumishi wako wanaoishi wakikutii kwa moyo wao wote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akasema: “Ee BWANA, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe mbinguni juu wala duniani chini, wewe unayetunza Agano lako la upendo na watumishi wanaodumu katika njia yako kwa moyo wote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akasema: “Ee bwana, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe juu mbinguni wala chini duniani, wewe unayetunza Agano lako la upendo na watumishi wanaodumu katika njia yako kwa moyo wote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akasema, Ee BWANA, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe, mbinguni, wala duniani; ushikaye maagano na rehema kwa watumishi wako, waendao mbele zako kwa moyo wao wote;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Aliomba akisema, “Ee, Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu mwingine kama wewe, mbinguni ama duniani. Wewe ni mwaminifu, kwani umetimiza agano lako na kuwaonesha fadhili zako watumishi wako wanaoishi wakikutii kwa moyo wao wote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akasema: Bwana Mungu wa Isiraeli, hakuna Mungu afananaye na wewe, wala mbinguni wala nchini. Unawashikia watumishi wako agano lako na upole wako, wakiendelea mbele yako kwa mioyo yao yote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akasema, Ee BWANA, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe, mbinguni, wala duniani; ushikaye maagano na rehema kwa watumishi wako, waendao mbele zako kwa moyo wao wote;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Aliomba akisema: “Ee, Yawe, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu mwingine kama wewe, mbinguni au katika dunia. Wewe ni mwaminifu, maana umetimiza agano lako na kutenda mema kwa watumishi wako wanaoishi wakikutii kwa moyo wao wote.