2 Chronicles 6:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Lakini, ee Mungu kweli utakaa humu duniani na binadamu? Hata mbingu zenyewe, wala mbingu za mbingu za juu sana hazikutoshi, itakutoshaje nyumba hii ambayo nimeijenga?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Lakini kweli, je, Mungu atafanya makao duniani na wanadamu? Mbingu, hata mbingu zilizo juu sana, haziwezi kukutosha wewe. Sembuse Hekalu hili nililojenga!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini Mungu je! Yamkini atakaa na watu duniani? Tazama, mbingu na mbingu za mbingu za mbingu hazikutoshi; siuze nyumba hii niliyoijenga!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Lakini, ee Mungu kweli utakaa humu duniani na binadamu? Hata mbingu zenyewe, wala mbingu za mbingu za juu sana hazikutoshi, itakutoshaje nyumba hii ambayo nimeijenga?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Lakini kweli, je, Mungu atafanya makao duniani? Mbingu, hata mbingu zilizo juu sana, haziwezi kukutosha wewe. Sembuse Hekalu hili nililojenga!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Lakini kweli, je, Mungu atafanya makao duniani na wanadamu? Mbingu, hata mbingu zilizo juu sana, haziwezi kukutosha wewe. Sembuse Hekalu hili nililojenga!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini Mungu je! Yamkini atakaa na watu duniani? Tazama, mbingu na mbingu za mbingu za mbingu hazikutoshi; sembuse nyumba hii niliyoijenga!
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Lakini, ee Mungu kweli utakaa humu duniani na binadamu? Hata mbingu zenyewe, wala mbingu za mbingu za juu sana hazikutoshi, itakutoshaje nyumba hii ambayo nimeijenga?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Inakuwaje? Mungu anakaa kweli na watu huku nchini? Tazama! Mbingu nazo mbingu zilizoko juu ya mbingu hazikuenei, sembuse Nyumba hii, niliyoijenga!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini Mungu je! Yamkini atakaa na watu duniani? Tazama, mbingu na mbingu za mbingu za mbingu hazikutoshi; siuze nyumba hii niliyoijenga!
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Lakini, ee Mungu kweli utakaa humu katika dunia na wanadamu, ikiwa hata mbingu zenyewe, wala mbingu za mbingu za juu sana hazikutoshi? Namna gani nyumba hii ambayo nimejenga itakutoshelea?