2 Chronicles 6:20 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ichunge nyumba hii mchana na usiku, mahali ambapo umechagua watu wako waliabudu jina lako. Unisikie mimi mtumishi wako ninapokuja mahali hapa kuomba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Macho yako na yafumbuke kuelekea Hekalu hili usiku na mchana, mahali hapa ambapo ulisema, ‘Jina langu litakuwako humo,’ ili upate kusikia maombi ambayo mtumishi wako ataomba kuelekea mahali hapa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ili macho yako yafumbuke kwa nyumba hii mchana na usiku, mahali uliponena, ndipo utakapoliweka jina lako; usikie maombi atakayoomba mtumwa wako, akikabili mahali hapa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ichunge nyumba hii mchana na usiku, mahali ambapo umechagua watu wako waliabudu jina lako. Unisikie mimi mtumishi wako ninapokuja mahali hapa kuomba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Macho yako na yafumbuke kuelekea Hekalu hili usiku na mchana, mahali hapa ambapo ulisema, ‘Jina langu litakuwako humo,’ ili kwamba upate kusikia maombi ambayo mtumishi wako ataomba kuelekea mahali hapa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Macho yako na yafumbuke kuelekea Hekalu hili usiku na mchana, mahali hapa ambapo ulisema, ‘Jina langu litakuwako humo,’ ili kwamba upate kusikia maombi ambayo mtumishi wako ataomba kuelekea mahali hapa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ili macho yako yafumbuke juu ya nyumba hii mchana na usiku, mahali uliponena, ndipo utakapoliweka jina lako; usikie maombi atakayoomba mtumishi wako, akikabili mahali hapa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ichunge nyumba hii mchana na usiku, mahali ambapo umechagua watu wako waliabudu jina lako. Unisikie mimi mtumishi wako ninapokuja mahali hapa kuomba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Uwe macho kuiangalia Nyumba hii mchana na usiku, ipate kuwa mahali pale, uliposema: Mahali hapa ndipo, Jina langu litakapokuwa! Kwa hiyo yasikie maombo, mtumishi wako atakayokuomba mahali hapa!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ili macho yako yafumbuke kwa nyumba hii mchana na usiku, mahali uliponena, ndipo utakapoliweka jina lako; usikie maombi atakayoomba mtumwa wako, akikabili mahali hapa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Uchunge nyumba hii muchana na usiku pahali ambapo umechagua watu wako waliabudie jina lako. Unisikilize mimi mutumishi wako ninapokuja pahali hapa kuomba.