2 Chronicles 6:28 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Iwapo kuna njaa nchini au tauni, ukame, ugonjwa wa mimea, nzige au viwavi, au ikiwa watu wako wamezingirwa na maadui zao katika mji wao wowote ule; ikiwa kuna pigo lolote au ugonjwa wowote,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Njaa au tauni vikija katika nchi, au koga au kawa, nzige au panzi, au adui atakapowazingira katika mji wao wowote, maafa ya namna yoyote au ugonjwa wowote unaoweza kuwajia,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikiwa nchi imeingia njaa, au tauni, au ukosefu wa mvua, au ukungu, au nzige, au panzi; ikiwa adui wamewahusuru katika nchi ya miji yao, au ukiwapo msiba wo wote, au uele wo wote;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Iwapo kuna njaa nchini au tauni, ukame, ugonjwa wa mimea, nzige au viwavi, au ikiwa watu wako wamezingirwa na maadui zao katika mji wao wowote ule; ikiwa kuna pigo lolote au ugonjwa wowote,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Wakati njaa au tauni vikija juu ya nchi, au koga au kawa, nzige au panzi, au wakati adui atakapowazingira katika mji wao wo wote, maafa ya namna yo yote au ugonjwa wo wote unaoweza kuwajia,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Wakati njaa au tauni vikija juu ya nchi, au koga au kawa, nzige au panzi, au wakati adui atakapowazingira katika mji wao wowote, maafa ya namna yoyote au ugonjwa wowote unaoweza kuwajia,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikiwa nchi imeingia njaa, au tauni, au ukame, au ukungu, au nzige, au panzi; ikiwa adui wamewahusuru katika nchi ya miji yao, au ukiwapo msiba wowote, au ugonjwa wowote;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Iwapo kuna njaa nchini au tauni, ukame, ugonjwa wa mimea, nzige au viwavi, au ikiwa watu wako wamezingirwa na maadui zao katika mji wao wowote ule; ikiwa kuna pigo lolote au ugonjwa wowote,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Itakuwa, njaa iingie katika nchi hii au magonjwa mabaya, itakuwa, jua kali linyaushe mashamba yote, itakuwa, nzige na funutu wamalize vilaji vyote, itakuwa, adui zao wawasonge watu kwao malangoni mwao, itakuwa, mapigo menginemengine na magonjwa yo yote yawapate,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikiwa nchi imeingia njaa, au tauni, au ukosefu wa mvua, au ukungu, au nzige, au panzi; ikiwa adui wamewahusuru katika nchi ya miji yao, au ukiwapo msiba wo wote, au uele wo wote;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Ikiwa kuna njaa katika inchi au ugonjwa mukali, ukosefu wa mvua, ugonjwa wa mimea, nzige au vidudu vingine, au ikiwa watu wako wakishambuliwa na waadui zao katika muji wao wowote, ikiwa kuna pigo lolote au ugonjwa wowote,