2 Chronicles 6:29 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
tafadhali usikie maombi yoyote yatakayoombwa na mtu yeyote au watu wako wote wa Israeli, kila mtu akijua taabu yake na huzuni yake akikuomba huku akinyosha mikono yake kuelekea nyumba hii.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kila dua au ombi litakalotolewa na yeyote kati ya watu wako Israeli, akitambua taabu zake na uchungu wake, naye akainyoosha mikono yake kuelekea Hekalu hili,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
yo yote atakayoyaomba na kusihi mtu awaye yote, au watu wako Israeli wote pamoja, watakaojua kila mtu pigo lake mwenyewe, na msiba wake mwenyewe, akiinyoshea mikono nyumba hii;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
tafadhali usikie maombi yoyote yatakayoombwa na mtu yeyote au watu wako wote wa Israeli, kila mtu akijua taabu yake na huzuni yake akikuomba huku akinyosha mikono yake kuelekea nyumba hii.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
wakati dua au maombi yatakapofanywa na mmojawapo wa watu wako Israeli, kila mmoja akijua juu ya taabu ya moyo wake mwenyewe, akainyosha mikono yake kuelekea Hekalu hili,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
wakati dua au maombi yatakapofanywa na mmojawapo wa watu wako Israeli, kila mmoja akitambua taabu zake na uchungu wake, naye akainyoosha mikono yake kuelekea Hekalu hili,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
yoyote atakayoyaomba na kusihi mtu awaye yote, au watu wako Israeli wote pamoja, watakaojua kila mtu pigo lake mwenyewe, na msiba wake mwenyewe, akiinyoshea mikono nyumba hii;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
tafadhali usikie maombi yoyote yatakayoombwa na mtu yeyote au watu wako wote wa Israeli, kila mtu akijua taabu yake na huzuni yake akikuomba huku akinyosha mikono yake kuelekea nyumba hii.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
basi, lisikie kila ombo na kila lalamiko litakalokutokea, kama ni la mtu awaye yote, au la watu wote walio ukoo wako wa Waisiraeli, kwa kuwa kila mtu anayajua mapigo yake na maumivu yake! Hapo, watakapokuja kuikunjua mikono yao humu Nyumbani,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
yo yote atakayoyaomba na kusihi mtu awaye yote, au watu wako Israeli wote pamoja, watakaojua kila mtu pigo lake mwenyewe, na msiba wake mwenyewe, akiinyoshea mikono nyumba hii;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
tafazali usikilize maombi yoyote yatakayoombwa na mutu yeyote au watu wako wote Waisraeli, kila mutu akijua taabu yake na huzuni yake akikuomba naye akinyoosha mikono yake kuelekea nyumba hii,