2 Chronicles 6:32 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Vivyo hivyo wakati mgeni asiye mmoja wa watu wako Israeli atakuja kutoka nchi ya mbali kwa ajili ya jina lako kuu, na kwa sababu ya nguvu na ulinzi wako, kuomba katika nyumba hii,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kwa habari ya mgeni ambaye si miongoni mwa watu wako Israeli, lakini amekuja kutoka nchi ya mbali kwa sababu ya jina lako kuu na mkono wako wenye nguvu ulionyooshwa, atakapokuja kuomba kuelekea Hekalu hili,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata na mgeni naye, asiyekuwa mmoja wa watu wako Israeli, atakapokuja kutoka nchi iliyo mbali sana kwa ajili ya jina lako kuu, na mkono wako ulio hodari, na mkono wako ulionyoshwa; hao watakapokuja na kuomba wakiielekea nyumba hii;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Vivyo hivyo wakati mgeni asiye mmoja wa watu wako Israeli atakuja kutoka nchi ya mbali kwa ajili ya jina lako kuu, na kwa sababu ya nguvu na ulinzi wako, kuomba katika nyumba hii,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kwa habari ya mgeni ambaye si miongoni mwa watu wako Israeli, lakini amekuja kutoka nchi ya mbali kwa sababu ya jina lako kuu na mkono wako wenye nguvu ulionyoshwa, atakapokuja kuomba akikabili Hekalu hili,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kwa habari ya mgeni ambaye si miongoni mwa watu wako Israeli, lakini amekuja kutoka nchi ya mbali kwa sababu ya jina lako kuu na mkono wako wenye nguvu ulionyooshwa, atakapokuja kuomba kuelekea Hekalu hili,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata na mgeni naye, asiyekuwa mmoja wa watu wako Israeli, atakapokuja kutoka nchi iliyo mbali sana kwa ajili ya jina lako kuu, na mkono wako ulio hodari, na mkono wako ulionyoshwa; hao watakapokuja na kuomba wakiielekea nyumba hii;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Vivyo hivyo wakati mgeni asiye mmoja wa watu wako Israeli atakuja kutoka nchi ya mbali kwa ajili ya jina lako kuu, na kwa sababu ya nguvu na ulinzi wako, kuomba katika nyumba hii,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena itakuwa, hata mgeni asiye wa ukoo wako wa Waisiraeli aje huku na kutoka katika nchi ya mbali kwa ajili ya Jina lako lililo kuu na kwa ajili ya kiganja chako kilicho na nguvu na kwa ajili ya mkono wako uliokunjuka; basi, hapo watakapokuja, waombee humu Nyumbani,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata na mgeni naye, asiyekuwa mmoja wa watu wako Israeli, atakapokuja kutoka nchi iliyo mbali sana kwa ajili ya jina lako kuu, na mkono wako ulio hodari, na mkono wako ulionyoshwa; hao watakapokuja na kuomba wakiielekea nyumba hii;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Na hata mugeni asiyekuwa Mwisraeli atakayekuja kutoka inchi ya mbali kwa ajili ya jina lako kubwa, na juu ya nguvu na ulinzi wako, akikuja kuomba katika nyumba hii,