2 Chronicles 6:33 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
nakusihi umsikie toka huko kwako mbinguni, na umjalie huyo mgeni yote atakayokuomba kusudi watu wote ulimwenguni wapate kujua jina lako na kukutii kama wafanyavyo watu wako Israeli na wapate kufahamu kwamba nyumba hii ambayo nimeijenga inajulikana kwa jina lako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
basi na usikie ukiwa mbinguni, makao yako, ukafanye lolote ambalo mgeni huyo anakuomba, ili mataifa yote ya dunia wapate kujua jina lako na wakuogope kama wafanyavyo watu wako Israeli, nao wapate pia kujua kwamba nyumba hii niliyoijenga imeitwa kwa Jina lako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
basi usikie huko mbinguni, toka makaoni mwako, ukatende yote atakayokuomba huyo mgeni; ili watu wote wa dunia wapate kulijua jina lako, na kukucha wewe, kama watu wako Israeli, tena wajue ya kuwa nyumba hii niliyoijenga imeitwa kwa jina lako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
nakusihi umsikie toka huko kwako mbinguni, na umjalie huyo mgeni yote atakayokuomba kusudi watu wote ulimwenguni wapate kujua jina lako na kukutii kama wafanyavyo watu wako Israeli na wapate kufahamu kwamba nyumba hii ambayo nimeijenga inajulikana kwa jina lako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
basi na usikie kutoka mbinguni, mahali pa makao yako, ukafanye lo lote ambalo mgeni huyo anakuomba, ili mataifa yote ya dunia wapate kujua jina lako na wakuogope kama wafanyavyo watu wako Israeli nao wapate pia kujua kwamba nyumba hii niliyoijenga imeitwa kwa Jina lako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
basi na usikie kutoka mbinguni, mahali pa makao yako, ukafanye lolote ambalo mgeni huyo anakuomba, ili mataifa yote ya dunia wapate kujua jina lako na wakuogope kama wafanyavyo watu wako Israeli nao wapate pia kujua kwamba nyumba hii niliyoijenga imeitwa kwa Jina lako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
basi usikie huko mbinguni, toka makaoni mwako, ukatende yote atakayokuomba huyo mgeni; ili watu wote wa dunia wapate kulijua jina lako, na kukucha wewe, kama watu wako Israeli, tena wajue ya kuwa nyumba hii niliyoijenga imeitwa kwa jina lako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
nakusihi umsikie toka huko kwako mbinguni, na umjalie huyo mgeni yote atakayokuomba kusudi watu wote ulimwenguni wapate kujua jina lako na kukutii kama wafanyavyo watu wako Israeli na wapate kufahamu kwamba nyumba hii ambayo nimeijenga inajulikana kwa jina lako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wewe na uwasikie huko mbinguni kuliko na Kao lako la kukaa, uyafanye yote, yule mgeni atakayokuomba na kukulilia, makabila yote ya nchi yalijue Jina lako, wakuogope kama wao walio ukoo wako wa Waisiraeli, tena wajue, ya kuwa Nyumba hii, niliyoijenga, imeitwa kwa Jina lako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
basi usikie huko mbinguni, toka makaoni mwako, ukatende yote atakayokuomba huyo mgeni; ili watu wote wa dunia wapate kulijua jina lako, na kukucha wewe, kama watu wako Israeli, tena wajue ya kuwa nyumba hii niliyoijenga imeitwa kwa jina lako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
ninakusihi umusikilize toka kule kwako mbinguni, na umujalie yule mugeni yote atakayokuomba kusudi watu wote katika ulimwengu wapate kujua jina lako na kukutii kama vile watu wako Waisraeli walivyofanya na wapate kufahamu kwamba nyumba hii ambayo nimejenga inajulikana kwa jina lako.