2 Chronicles 6:38 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
pia kama watatubu kwa moyo wao wote na kwa roho yao yote wakati watakapokuwa katika nchi ya uhamisho, na kama watakuomba wakielekea nchi yao ambayo uliwapatia babu zao, mji huu ambao uliuchagua na nyumba hii ambayo nimeijenga kwa ajili ya jina lako;
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
wakikugeukia kwa moyo wao wote na nafsi zao katika nchi ya adui zao ambao waliwachukua mateka, wakakuomba kuelekea nchi uliyowapa baba zao, kuelekea mji uliouchagua na Hekalu nililolijenga kwa ajili ya Jina lako,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wakurudiapo kwa mioyo yao yote, na kwa nia zao zote, katika nchi ya uhamisho wao, adui walikowahamisha, wakiomba na kuielekea nchi uliyowapa baba zao, na mji huu uliouchagua, na nyumba hii niliyoijenga kwa jina lako;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
pia kama watatubu kwa moyo wao wote na kwa roho yao yote wakati watakapokuwa katika nchi ya uhamisho, na kama watakuomba wakielekea nchi yao ambayo uliwapatia babu zao, mji huu ambao uliuchagua na nyumba hii ambayo nimeijenga kwa ajili ya jina lako;
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kama wakikugeukia kwa moyo wao wote na nafsi zao katika nchi ya adui zao ambao waliwachukua mateka, wakakuomba kuelekea nchi uliyowapa baba zao, kuelekea mji uliouchagua na Hekalu nililolijenga kwa ajili ya Jina lako,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kama wakikugeukia kwa moyo wao wote na nafsi zao katika nchi ya adui zao ambao waliwachukua mateka, wakakuomba kuelekea nchi uliyowapa baba zao, kuelekea mji uliouchagua na Hekalu nililolijenga kwa ajili ya Jina lako,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wakurudiapo kwa mioyo yao yote, na kwa nia zao zote, katika nchi ya uhamisho wao, adui walikowahamisha, wakiomba na kuielekea nchi uliyowapa baba zao, na mji huu uliouchagua, na nyumba hii niliyoijenga kwa jina lako;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
pia kama watatubu kwa moyo wao wote na kwa roho yao yote wakati watakapokuwa katika nchi ya uhamisho, na kama watakuomba wakielekea nchi yao ambayo uliwapatia babu zao, mji huu ambao uliuchagua na nyumba hii ambayo nimeijenga kwa ajili ya jina lako;
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
watakapokurudia hivyo kwa mioyo yao yote na kwa roho zao zote katika nchi ya uhamisho wao, walikohamishiwa, watakapokuomba na kuielekea nchi yao, uliyowapa baba zao, na mji, uliouchagua, na Nyumba hii, niliyolijengea Jina lako,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wakurudiapo kwa mioyo yao yote, na kwa nia zao zote, katika nchi ya uhamisho wao, adui walikowahamisha, wakiomba na kuielekea nchi uliyowapa baba zao, na mji huu uliouchagua, na nyumba hii niliyoijenga kwa jina lako;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
tena kama watatubu kwa moyo wao wote na kwa roho yao yote wakati watakapokuwa katika inchi ya uhamisho, na kama watakuomba wakielekea inchi yao ambayo uliwapatia babu zao, muji huu ambao uliuchagua na nyumba hii ambayo nimeijenga kwa ajili ya jina lako,