2 Chronicles 6:41 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa inuka ee Bwana Mungu, uingie mahali pako pa kupumzika wewe pamoja na sanduku la agano la nguvu zako. Makuhani wako ee Bwana Mungu, wapate wokovu, na watakatifu wako wafurahie wema wako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Sasa inuka, Ee Bwana Mwenyezi Mungu, na uje mahali pako pa kupumzikia, wewe na Sanduku la nguvu zako. Makuhani wako, Ee Bwana Mwenyezi Mungu, na wavikwe wokovu, watakatifu wako na wafurahi katika wema wako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sasa, Ee Bwana, Mungu, uondoke, uende kwenye raha yako, wewe na sanduku la nguvu zako; makuhani wako, Ee Bwana, Mungu, wavikwe wokovu, watakatifu wako na washangilie mema.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa inuka ee Bwana Mungu, uingie mahali pako pa kupumzika wewe pamoja na sanduku la agano la nguvu zako. Makuhani wako ee Bwana Mungu, wapate wokovu, na watakatifu wako wafurahie wema wako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Sasa inuka, Ee BWANA Mungu, na uje mahali pako pa kupumzika, wewe na Sanduku la nguvu zako. Makuhani wako, Ee BWANA Mungu, na wavikwe wokovu, watakatifu wako na wafurahi katika wema wako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Sasa inuka, Ee bwana Mwenyezi Mungu, na uje mahali pako pa kupumzikia, wewe na Sanduku la nguvu zako. Makuhani wako, Ee bwana Mwenyezi Mungu, na wavikwe wokovu, watakatifu wako na wafurahi katika wema wako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sasa, Ee BWANA, Mungu, uondoke, uende kwenye raha yako, wewe na sanduku la nguvu zako; makuhani wako, Ee BWANA, Mungu, wavikwe wokovu, watakatifu wako na washangilie mema.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sasa inuka ee Bwana Mungu, uingie mahali pako pa kupumzika wewe pamoja na sanduku la agano la nguvu zako. Makuhani wako ee Bwana Mungu, wapate wokovu, na watakatifu wako wafurahie wema wako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa inuka, Bwana Mungu, uingie hapa, ndipo utulie na Sanduku lililo na nguvu yako! Watambikaji wako, Bwana Mungu, na wavikwe wokovu, nao wakuchao wayafurahie mema!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sasa, Ee BWANA, Mungu, uondoke, uende kwenye raha yako, wewe na sanduku la nguvu zako; makuhani wako, Ee BWANA, Mungu, wavikwe wokovu, watakatifu wako na washangilie mema.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Sasa, ee Yawe, Mungu, uingie pahali pako pa kupumzika, wewe pamoja na Sanduku la Agano la nguvu zako. “Ee Yawe, Mungu, makuhani wako wapate wokovu, na watakatifu wako wafurahie uzuri wako.