2 Chronicles 7:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Solomoni alipomaliza sala yake, moto ulishuka kutoka mbinguni na kuchoma sadaka na tambiko za kuteketeza zilizotolewa, kisha utukufu wa Mwenyezi-Mungu ukaijaza nyumba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya Sulemani kumaliza kuomba, moto ukashuka kutoka mbinguni na kuteketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu, nao utukufu wa Mwenyezi Mungu ukalijaza Hekalu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Sulemani alipokwisha maombi hayo, moto ukashuka kutoka mbinguni, ukateketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu; utukufu wa Bwana ukaijaza nyumba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Solomoni alipomaliza sala yake, moto ulishuka kutoka mbinguni na kuchoma sadaka na tambiko za kuteketeza zilizotolewa, kisha utukufu wa Mwenyezi-Mungu ukaijaza nyumba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya Solomoni kumaliza kuomba, moto ukashuka kutoka mbinguni na kuteketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu, nao utukufu wa BWANA ukalijaza Hekalu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya Sulemani kumaliza kuomba, moto ukashuka kutoka mbinguni na kuteketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu, nao utukufu wa bwana ukalijaza Hekalu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Sulemani alipomaliza maombi hayo, moto ukashuka kutoka mbinguni, ukateketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu; utukufu wa BWANA ukaijaza nyumba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Solomoni alipomaliza sala yake, moto ulishuka kutoka mbinguni na kuchoma sadaka na tambiko za kuteketeza zilizotolewa, kisha utukufu wa Mwenyezi-Mungu ukaijaza nyumba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Salomo alipokwisha kuomba, ndipo, moto uliposhuka toka mbinguni, ukala ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima na ng'ombe nyingine za tambiko, kisha utukufu wa Bwana ukajaa mle Nyumbani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Sulemani alipokwisha maombi hayo, moto ukashuka kutoka mbinguni, ukateketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu; utukufu wa BWANA ukaijaza nyumba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Solomono alipomaliza maombi yake, moto ukashuka kutoka mbinguni na kuchoma sadaka na sadaka za kuteketeza kwa moto zilizotolewa, kisha utukufu wa Yawe ukajaza nyumba.