2 Chronicles 7:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku iliyofuata ambayo ilikuwa siku ya ishirini na tatu ya mwezi wa saba, Solomoni aliwaaga watu waende kwao, wakishangilia na kufurahi moyoni kwa sababu ya wema ambao Mwenyezi-Mungu aliowajalia Daudi, Solomoni na watu wake Israeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika siku ya ishirini na tatu ya mwezi wa saba Sulemani akawaaga watu waende nyumbani mwao, wakishangilia na kufurahi mioyoni mwao, kwa wema mwingi Mwenyezi Mungu aliomtendea Daudi na Sulemani na kwa ajili ya watu wake Israeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaruhusu watu waende hemani kwao siku ya ishirini na tatu, ya mwezi wa saba, wakifurahi na kuchangamka mioyoni kwa wema wote Bwana aliomfanyia Daudi, na Sulemani, na Israeli watu wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku iliyofuata ambayo ilikuwa siku ya ishirini na tatu ya mwezi wa saba, Solomoni aliwaaga watu waende kwao, wakishangilia na kufurahi moyoni kwa sababu ya wema ambao Mwenyezi-Mungu aliowajalia Daudi, Solomoni na watu wake Israeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika siku ya ishirini na tatu ya mwezi wa saba Solomoni akawaaga watu waende nyumbani mwao, wakishangilia na kufurahi mioyoni mwao, kwa wema mwingi BWANA Mungu aliomtendea Daudi na Solomoni na kwa ajili ya watu wake Israeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika siku ya ishirini na tatu ya mwezi wa saba Sulemani akawaaga watu waende nyumbani mwao, wakishangilia na kufurahi mioyoni mwao, kwa wema mwingi bwana Mwenyezi Mungu aliomtendea Daudi na Sulemani na kwa ajili ya watu wake Israeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawaruhusu watu waende hemani kwao siku ya ishirini na tatu, ya mwezi wa saba, wakifurahi na kuchangamka mioyoni kwa wema wote BWANA aliomfanyia Daudi, na Sulemani, na Israeli watu wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku iliyofuata ambayo ilikuwa siku ya ishirini na tatu ya mwezi wa saba, Solomoni aliwaaga watu waende kwao, wakishangilia na kufurahi moyoni kwa sababu ya wema ambao Mwenyezi-Mungu aliowajalia Daudi, Solomoni na watu wake Israeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku ya ishirini na tatu ya mwezi wa saba akawapa watu ruhusa kwenda mahemani kwao, wakifurahi na kuchangamka mioyoni kwa wema, Bwana aliomfanyizia Dawidi naye Salomo nao walio ukoo wake wa Waisiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaruhusu watu waende hemani kwao siku ya ishirini na tatu, ya mwezi wa saba, wakifurahi na kuchangamka mioyoni kwa wema wote BWANA aliomfanyia Daudi, na Sulemani, na Israeli watu wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku iliyofuata ambayo ilikuwa siku ya makumi mbili na tatu ya mwezi wa saba, Solomono akawaaga watu waende kwao, wakishangilia na kufurahi ndani ya moyo kwa sababu ya mazuri ambayo Yawe alimutendea Daudi, Solomono na kwa watu wake Waisraeli.