2 Chronicles 7:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
kama watu hao wangu wakijinyenyekesha, wakasali, wakanitafuta na kuacha njia zao mbaya, basi, mimi nitawasikiliza kutoka juu mbinguni; nitawasamehe dhambi yao na kuistawisha nchi yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
ikiwa watu wangu, wanaoitwa kwa Jina langu, watajinyenyekeza na kuomba na kuutafuta uso wangu, na kuacha njia zao mbaya, basi nitasikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi yao, na nitaiponya nchi yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
kama watu hao wangu wakijinyenyekesha, wakasali, wakanitafuta na kuacha njia zao mbaya, basi, mimi nitawasikiliza kutoka juu mbinguni; nitawasamehe dhambi yao na kuistawisha nchi yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kama watu wangu, wanaoitwa kwa Jina langu, watajinyenyekesha na kuomba na kuutafuta uso wangu na kuacha njia zao mbaya, basi nitasikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi yao na nitaiponya nchi yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kama watu wangu, wanaoitwa kwa Jina langu, watajinyenyekesha na kuomba na kuutafuta uso wangu na kuacha njia zao mbaya, basi nitasikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi yao na nitaiponya nchi yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekeza, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
kama watu hao wangu wakijinyenyekesha, wakasali, wakanitafuta na kuacha njia zao mbaya, basi, mimi nitawasikiliza kutoka juu mbinguni; nitawasamehe dhambi yao na kuistawisha nchi yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
basi, wao walio ukoo wangu, walioitwa kwa Jina langu, watakaponyenyekea na kuniomba wakiutafuta uso wangu, warudi na kuziacha njia zao mbaya, ndipo, nitakapowasikia huko mbinguni, niwaondolee makosa yao, niiponye hii nchi yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
kama watu wangu hao wakijinyenyekeza, wakiomba, wakinitafuta na kuacha njia zao mbaya, basi, mimi nitawasikiliza kutokea juu mbinguni, nitawasamehe zambi yao na kustawisha inchi yao.