2 Chronicles 7:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
kwa sababu hiyo mimi nitawangoeni kutoka nchi hii ambayo nimewapa. Kadhalika na nyumba hii ambayo nimeiweka wakfu kwa ajili ya jina langu nitaitupilia mbali nami, na kuifanya kitu cha kupuuzwa na kudharauliwa miongoni mwa mataifa yote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
ndipo nitakapoing’oa Israeli kutoka nchi yangu niliyowapa, nami nitalikataa Hekalu hili nililolitakasa kwa ajili ya Jina langu. Nitalifanya kitu cha kudharauliwa na kitu cha kudhihakiwa miongoni mwa watu wote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ndipo nitawang'oa katika nchi yangu niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaiondosha itoke mbele zangu, nami nitaifanya kuwa mithali na tukano katikati ya watu wote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
kwa sababu hiyo mimi nitawang'oeni kutoka nchi hii ambayo nimewapa. Kadhalika na nyumba hii ambayo nimeiweka wakfu kwa ajili ya jina langu nitaitupilia mbali nami, na kuifanya kitu cha kupuuzwa na kudharauliwa miongoni mwa mataifa yote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
ndipo nitakapoing'oa Israeli kutoka katika nchi yangu niliyowapa, nami nitalikataa Hekalu hili nililolitakasa kwa ajili ya Jina langu. Nitalifanya kitu cha kudharauliwa na kitu cha kudhihakiwa miongoni mwa mataifa yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
ndipo nitakapoing’oa Israeli kutoka nchi yangu niliyowapa, nami nitalikataa Hekalu hili nililolitakasa kwa ajili ya Jina langu. Nitalifanya kitu cha kudharauliwa na kitu cha kudhihakiwa miongoni mwa watu wote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ndipo nitawang'oa katika nchi yangu niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaiondosha itoke mbele zangu, nami nitaifanya kuwa mithali na tukano katikati ya watu wote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
kwa sababu hiyo mimi nitawangoeni kutoka nchi hii ambayo nimewapa. Kadhalika na nyumba hii ambayo nimeiweka wakfu kwa ajili ya jina langu nitaitupilia mbali nami, na kuifanya kitu cha kupuuzwa na kudharauliwa miongoni mwa mataifa yote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ndipo, nitakapowang'oa katika hii nchi yangu, niliyowapa, nayo Nyumba hii, niliyoitakasa kuwa Kao la Jina langu, nitaitupa, macho yangu yasiione tena, nitaitoa kuwa fumbo na simango kwa makabila yote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ndipo nitawang’oa katika nchi yangu niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaiondosha itoke mbele zangu, nami nitaifanya kuwa mithali na tukano katikati ya watu wote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
kwa sababu hiyo mimi nitawaongoa kutoka katika inchi hii ambayo nimewapa. Vielvile na nyumba hii ambayo nimeitakasa kwa ajili ya jina langu nitaitupilia mbali nami, na kuifanya kitu cha kuchekelewa na kuzarauliwa kati ya mataifa yote.”