2 Chronicles 7:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na juu ya nyumba hii ambayo nimetukuka, kila apitaye karibu atashtuka na kuuliza, ‘Kwa nini Mwenyezi-Mungu amefanya hivyo kwa nchi hii na kwa nyumba hii?’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ingawa Hekalu hili linavutia sana sasa, wote watakaolipita watashangaa na kusema, ‘Kwa nini Mwenyezi Mungu amefanya kitu kama hiki katika nchi hii na kwa Hekalu hili?’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na nyumba hii, iliyo juu, kila apitaye ataona ushangao, atasema, Mbona Bwana ameitendea hivi nchi hii, na nyumba hii?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na juu ya nyumba hii ambayo nimetukuka, kila apitaye karibu atashtuka na kuuliza, ‘Kwa nini Mwenyezi-Mungu amefanya hivyo kwa nchi hii na kwa nyumba hii?’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ingawa Hekalu hili sasa ni la fahari sana, wale wote watakaopita watashangaa na kusema, ‘Kwa nini BWANA amefanya kitu kama hiki katika nchi hii na kwa Hekalu hili?’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ingawa Hekalu hili linavutia sana sasa, wote watakaolipita watashangaa na kusema, ‘Kwa nini bwana amefanya kitu kama hiki katika nchi hii na kwa Hekalu hili?’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na nyumba hii, iliyo juu, kila apitaye ataona ushangao, atasema, Mbona BWANA ameitendea hivi nchi hii, na nyumba hii?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na juu ya nyumba hii ambayo nimetukuka, kila apitaye karibu atashtuka na kuuliza, ‘Kwa nini Mwenyezi-Mungu amefanya hivyo kwa nchi hii na kwa nyumba hii?’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nayo Nyumba hii iliyokuwa imetukuka kabisa, basi, kila atakayepita hapo ataistukia na kuuliza: Kwa sababu gani Bwana ameifanyizia hivi nchi hii na Nyumba hii?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na nyumba hii, iliyo juu, kila apitaye ataona ushangao, atasema, Mbona BWANA ameitendea hivi nchi hii, na nyumba hii?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Na juu ya nyumba hii ambayo nimetukuzwa, kila anayepita karibu atashituka na kuuliza: ‘Kwa nini Yawe amefanya hivyo kwa inchi hii na kwa nyumba hii?’