2 Chronicles 7:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wengine watajibu, ‘Ni kwa sababu walimwacha Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zao aliyewatoa nchini Misri; wakashikamana na miungu mingine, wakaiabudu na kuitumikia. Kwa hiyo Mwenyezi-Mungu amewaletea maafa haya yote.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu watajibu, ‘Ni kwa sababu wamemwacha Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zao, aliyewatoa Misri, nao wamekumbatia miungu mingine, wakaiabudu na kuitumikia, ndiyo sababu ameyaleta maafa haya yote juu yao.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao watajibu, Kwa sababu walimwacha Bwana, Mungu wa baba zao, aliyewaleta kutoka nchi ya Misri, wakashikamana na miungu mingine, wakaiabudu, na kuitumikia; kwa hiyo ameyaleta mabaya haya yote juu yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wengine watajibu, ‘Ni kwa sababu walimwacha Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zao aliyewatoa nchini Misri; wakashikamana na miungu mingine, wakaiabudu na kuitumikia. Kwa hiyo Mwenyezi-Mungu amewaletea maafa haya yote.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu watajibu, ‘Ni kwa sababu wamemwacha BWANA, Mungu wa baba zao, ambaye aliwatoa Misri, nao wamekumbatia miungu mingine, wakaiabudu na kuitumikia, hiyo ndiyo sababu alileta haya maafa yote juu yao.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu watajibu, ‘Ni kwa sababu wamemwacha bwana, Mungu wa baba zao, aliyewatoa Misri, nao wamekumbatia miungu mingine, wakaiabudu na kuitumikia, ndiyo sababu ameyaleta maafa haya yote juu yao.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao watajibu, Kwa sababu walimwacha BWANA, Mungu wa baba zao, aliyewaleta kutoka nchi ya Misri, wakashikamana na miungu mingine, wakaiabudu, na kuitumikia; kwa hiyo ameyaleta mabaya haya yote juu yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wengine watajibu, ‘Ni kwa sababu walimwacha Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zao aliyewatoa nchini Misri; wakashikamana na miungu mingine, wakaiabudu na kuitumikia. Kwa hiyo Mwenyezi-Mungu amewaletea maafa haya yote.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, watakapojibu: Kwa kuwa walimwacha Bwana Mungu wa baba zao aliyewatoa katika nchi ya Misri, wakashikamana na miungu mingine, wakaiangukia na kuitumikia, hii ndiyo sababu, akiwaletea haya mabaya yote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao watajibu, Kwa sababu walimwacha BWANA, Mungu wa baba zao, aliyewaleta kutoka nchi ya Misri, wakashikamana na miungu mingine, wakaiabudu, na kuitumikia; kwa hiyo ameyaleta mabaya haya yote juu yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wengine watajibu: ‘Ni kwa sababu walimwacha Yawe, Mungu wa babu zao aliyewatoa toka katika inchi ya Misri; wakashikamana na miungu mingine, wakaiabudu na kuitumikia. Kwa hiyo Yawe amewaletea hasara hizi zote.’ ”