2 Chronicles 7:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waisraeli wote walipoona moto ukishuka kutoka mbinguni na utukufu wa Mwenyezi-Mungu ulijaa katika nyumba walisujudu nyuso zao zikifika mpaka sakafuni, wakamwabudu na kumshukuru Mwenyezi-Mungu wakisema, “Kwa kuwa ni mwema, fadhili zake zadumu milele.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waisraeli wote walipoona moto ukishuka na utukufu wa Mwenyezi Mungu ukiwa juu ya Hekalu, wakapiga magoti sakafuni wakasujudu, nyuso zao zikigusa chini, wakamwabudu na kumshukuru Mwenyezi Mungu, wakisema, “Yeye ni mwema; fadhili zake zadumu milele.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakatazama wana wa Israeli wote, uliposhuka ule moto, utukufu wa Bwana ulipokuwapo juu ya nyumba; wakasujudu kifulifuli hata nchi sakafuni, wakaabudu, wakamshukuru Bwana, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waisraeli wote walipoona moto ukishuka kutoka mbinguni na utukufu wa Mwenyezi-Mungu ulijaa katika nyumba walisujudu nyuso zao zikifika mpaka sakafuni, wakamwabudu na kumshukuru Mwenyezi-Mungu wakisema, “Kwa kuwa ni mwema, fadhili zake zadumu milele.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waisraeli wote walipoona moto ukishuka na utukufu wa BWANA ukiwa juu ya Hekalu, wakapiga magoti sakafuni wakasujudu nyuso zao mpaka chini, nao wakamwabudu na kumshukuru BWANA wakisema, “Yeye ni mwema; upendo wake unadumu milele.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waisraeli wote walipoona moto ukishuka na utukufu wa bwana ukiwa juu ya Hekalu, wakapiga magoti sakafuni wakasujudu nyuso zao mpaka chini, nao wakamwabudu na kumshukuru bwana wakisema, “Yeye ni mwema; upendo wake unadumu milele.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wana wa Israeli wote walipoona ule moto ukishuka, utukufu wa BWANA ulipokuwa katika nyumba, wakasujudu kifudifudi mpaka sakafuni, wakaabudu, wakamshukuru BWANA, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waisraeli wote walipoona moto ukishuka kutoka mbinguni na utukufu wa Mwenyezi-Mungu ulijaa katika nyumba walisujudu nyuso zao zikifika mpaka sakafuni, wakamwabudu na kumshukuru Mwenyezi-Mungu wakisema, “Kwa kuwa ni mwema, fadhili zake zadumu milele.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wana wote wa Isiraeli walipoona, jinsi moto ulivyoshuka nao utukufu wa Bwana ulivyokaa juu ya Nyumba hii, wakapiga magoti na kujinamisha chini hapo palipopigiliwa mawe, wakamwangukia Bwana na kumshukuru, ya kuwa ni mwema, ya kuwa upole wake ni wa kale na kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakatazama wana wa Israeli wote, uliposhuka ule moto, utukufu wa BWANA ulipokuwapo juu ya nyumba; wakasujudu kifulifuli hata nchi sakafuni, wakaabudu, wakamshukuru BWANA, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waisraeli wote walipoona moto ukishuka kutoka mbinguni na utukufu wa Yawe katika nyumba, wakainama nyuso zao zikifika mpaka chini. Wakamwabudu na kumushukuru Yawe wakisema: “Yeye ni muzuri. Wema wake unadumu milele.”