2 Chronicles 7:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Makuhani walisimama mahali maalumu walipoagizwa kusimama, nao Walawi walisimama wakiwa na vyombo vya Mwenyezi-Mungu vya muziki mfalme Daudi alivyovitengeneza kwa ajili ya kutoa shukrani kwa Mwenyezi-Mungu. Waliimba, “Kwa kuwa fadhili zake zadumu milele,” Daudi alivyowaagiza. Makuhani walipiga tarumbeta hali Waisraeli wote walikuwa wamesimama.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Makuhani wakasimama kwenye nafasi zao, vivyo hivyo Walawi wakiwa na vyombo vya uimbaji vya Mwenyezi Mungu ambavyo Mfalme Daudi alikuwa ametengeneza kwa ajili ya kumsifu Mwenyezi Mungu, navyo vilitumika aliposhukuru, akisema, “Fadhili zake zadumu milele.” Mkabala na Walawi, makuhani walipiga tarumbeta zao, nao Waisraeli wote walikuwa wamesimama.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakasimama makuhani sawasawa na malinzi yao; Walawi nao pamoja na vinanda vya Bwana, alivyovifanya Daudi mfalme, ili kumshukuru Bwana, kwa maana fadhili zake ni za milele, hapo aliposifu Daudi kwa mikono yao; nao makuhani wakapiga panda mbele yao; nao Israeli wote wakasimama.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Makuhani walisimama mahali maalumu walipoagizwa kusimama, nao Walawi walisimama wakiwa na vyombo vya Mwenyezi-Mungu vya muziki mfalme Daudi alivyovitengeneza kwa ajili ya kutoa shukrani kwa Mwenyezi-Mungu. Waliimba, “Kwa kuwa fadhili zake zadumu milele,” Daudi alivyowaagiza. Makuhani walipiga tarumbeta hali Waisraeli wote walikuwa wamesimama.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Makuhani wakasimama kwenye nafasi zao, vivyo hivyo Walawi wakiwa na vyombo vya uimbaji vya BWANA ambavyo Mfalme Daudi alikuwa ametengeneza kwa ajili ya kumsifu BWANA, navyo vilitumika wakati aliposhukuru, akisema, “Upendo wake wadumu milele.” Mkabala na Walawi, makuhani walipiga tarumbeta zao, nao Waisraeli wote walikuwa wamesimama.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Makuhani wakasimama kwenye nafasi zao, vivyo hivyo Walawi wakiwa na vyombo vya uimbaji vya bwana ambavyo Mfalme Daudi alikuwa ametengeneza kwa ajili ya kumsifu bwana, navyo vilitumika wakati aliposhukuru, akisema, “Upendo wake wadumu milele.” Mkabala na Walawi, makuhani walipiga tarumbeta zao, nao Waisraeli wote walikuwa wamesimama.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Makuhani wakasimama kwenye nafasi zao walipoagizwa; Walawi nao pamoja na vinanda vya BWANA, alivyovifanya Daudi mfalme, ili kumshukuru BWANA, kwa maana fadhili zake ni za milele, hapo aliposifu Daudi kwa mikono yao; nao makuhani wakapiga panda mbele yao; nao Israeli wote wakasimama.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Makuhani walisimama mahali maalumu walipoagizwa kusimama, nao Walawi walisimama wakiwa na vyombo vya Mwenyezi-Mungu vya muziki mfalme Daudi alivyovitengeneza kwa ajili ya kutoa shukrani kwa Mwenyezi-Mungu. Waliimba, “Kwa kuwa fadhili zake zadumu milele,” Daudi alivyowaagiza. Makuhani walipiga tarumbeta hali Waisraeli wote walikuwa wamesimama.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watambikaji wakawa wakisimama na kuziangalia kazi zao, nao Walawi wakashika vyombo vya kumwimbia Bwana, mfalme Dawidi alivyovitengeneza hapo, alipomshangilia Bwana, navyo vikamshukuru Bwana kwamba: Upole wake ni wa kale na kale; nao watambikaji waliowaelekea wakapiga matarumbeta, nao Waisiraeli wote walikuwa wamesimama.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakasimama makuhani sawasawa na malinzi yao; Walawi nao pamoja na vinanda vya BWANA, alivyovifanya Daudi mfalme, ili kumshukuru BWANA, kwa maana fadhili zake ni za milele, hapo aliposifu Daudi kwa mikono yao; nao makuhani wakapiga panda mbele yao; nao Israeli wote wakasimama.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Makuhani walikuwa wakisimama kwenye nafasi za kazi zao, nao Walawi, walisimama wakiwa na vyombo vya Yawe vya muziki mufalme Daudi alivyotengeneza kwa ajili ya kutoa shukrani kwa Yawe. Waliimba: “Wema wake unadumu milele.” Wakati Daudi alipotoa shukrani, walimusaidia; makuhani walipiga baragumu nao Waisraeli wote wakasimama.