2 Chronicles 7:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye Solomoni kwa muda wa siku saba alifanya sikukuu pamoja na kusanyiko kubwa la watu wote wa Israeli waliotoka kiingilio cha Hamathi mpaka mto wa Misri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo Sulemani akaiadhimisha sikukuu wakati ule kwa muda wa siku saba, na Waisraeli wote pamoja naye. Walikuwa kusanyiko kubwa sana, watu kutoka Lebo-Hamathi hadi Kijito cha Misri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, wakati ule Sulemani akafanya sikukuu, na Israeli wote pamoja naye, kusanyiko kubwa sana, toka maingilio ya Hamathi mpaka kijito cha Misri, muda wa siku saba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye Solomoni kwa muda wa siku saba alifanya sikukuu pamoja na kusanyiko kubwa la watu wote wa Israeli waliotoka kiingilio cha Hamathi mpaka mto wa Misri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo Mfalme Solomoni akaadhimisha sikukuu wakati ule kwa muda wa siku saba, akiwa pamoja na Israeli wote, kusanyiko kubwa sana, watu kutoka Lebo-Hamathi hadi Wadi ya Misri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo Sulemani akaiadhimisha sikukuu wakati ule kwa muda wa siku saba, na Israeli wote pamoja naye. Walikuwa kusanyiko kubwa sana, watu kutoka Lebo-Hamathi hadi Kijito cha Misri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, wakati ule Sulemani akafanya sikukuu, na Israeli wote pamoja naye, kusanyiko kubwa sana, toka maingilio ya Hamathi mpaka kijito cha Misri, muda wa siku saba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye Solomoni kwa muda wa siku saba alifanya sikukuu pamoja na kusanyiko kubwa la watu wote wa Israeli waliotoka kiingilio cha Hamathi mpaka mto wa Misri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, Salomo alivyofanya wakati huo sikukuu ya siku saba, yeye pamoja nao Waisiraeli wote, wakawa mkutano mkubwa sana wa watu waliotoka Hamati mpaka kwenye mto wa Misri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, wakati ule Sulemani akafanya sikukuu, na Israeli wote pamoja naye, kusanyiko kubwa sana, toka maingilio ya Hamathi mpaka kijito cha Misri, muda wa siku saba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye Solomono kwa muda wa siku saba alifanya sikukuu pamoja na kusanyiko kubwa la watu wote wa Israeli waliotoka kwenye kiingilio cha Hamati mpaka kwenye muto wa Misri.