2 Chronicles 7:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku ya nane, walikusanyika wakafanya ibada maalumu baada ya muda wa siku saba walizotumia kuitakasa meza ya matoleo ya sadaka, na siku saba nyingine za sikukuu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika siku ya nane walifanya kusanyiko, kwa sababu walikuwa wameadhimisha kuwekwa wakfu kwa madhabahu kwa muda wa siku saba, na sikukuu kwa muda wa siku nyingine saba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata siku ya nane wakaita kusanyiko la makini; kwa maana walishika kuitakasa madhabahu siku saba, na sikukuu siku saba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku ya nane, walikusanyika wakafanya ibada maalumu baada ya muda wa siku saba walizotumia kuitakasa meza ya matoleo ya sadaka, na siku saba nyingine za sikukuu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika siku ya nane walifanya kusanyiko, kwa kuwa walikuwa wanaadhimisha kuwekwa wakfu kwa madhabahu kwa muda wa siku saba na sikukuu kwa muda wa siku nyingine saba zaidi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika siku ya nane walifanya kusanyiko, kwa kuwa walikuwa wanaadhimisha kuwekwa wakfu kwa madhabahu kwa muda wa siku saba na sikukuu kwa muda wa siku nyingine saba zaidi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Siku ya nane wakaita kusanyiko la makini; kwa maana waliadhimisha kuitakasa madhabahu siku saba, na sikukuu siku saba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku ya nane, walikusanyika wakafanya ibada maalumu baada ya muda wa siku saba walizotumia kuitakasa meza ya matoleo ya sadaka, na siku saba nyingine za sikukuu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku ya nane wakakusanyika tena kufanya sikukuu; kwani zile siku saba ndizo, walizoieneza meza ya kutambikia ng'ombe za tambiko, hii sikukuu nayo ikawa ya siku saba tena.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata siku ya nane wakaita kusanyiko la makini; kwa maana walishika kuitakasa madhabahu siku saba, na sikukuu siku saba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku ya nane, walikusanyika wakafanya sikukuu nyuma ya muda wa siku saba, walizotumia kwa kutakasa meza ya matoleo ya sadaka, na siku saba nyingine za sikukuu.