2 Chronicles 8:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Solomoni alimhamisha binti Farao mfalme wa Misri, kutoka mji wa Daudi, akampeleka kwenye nyumba aliyomjengea. Alisema, “Mke wangu hataishi katika nyumba ya Daudi mfalme wa Israeli, kwa maana mahali pote ambapo sanduku la Mwenyezi-Mungu limekuwa, ni patakatifu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sulemani akampandisha mke wake binti Farao kutoka Mji wa Daudi na kumleta jumba la kifalme alilokuwa amemjengea, kwa kuwa alisema, “Mke wangu hataishi katika jumba la kifalme la Daudi mfalme wa Israeli, kwa sababu mahali ambapo Sanduku la Mwenyezi Mungu limefika ni patakatifu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sulemani akamleta binti Farao kutoka mji wa Daudi mpaka nyumba aliyomjengea; kwa kuwa alisema, Mke wangu hatakaa nyumbani mwa Daudi mfalme wa Israeli, kwa kuwa ni patakatifu, mahali palipofika sanduku la Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Solomoni alimhamisha binti Farao mfalme wa Misri, kutoka mji wa Daudi, akampeleka kwenye nyumba aliyomjengea. Alisema, “Mke wangu hataishi katika nyumba ya Daudi mfalme wa Israeli, kwa maana mahali pote ambapo sanduku la Mwenyezi-Mungu limekuwa, ni patakatifu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Solomoni akampandisha mke wake binti wa Farao kutoka Mji wa Daudi mpaka kwenye jumba la kifalme alilokuwa amemjengea, kwa kuwa alisema, “Mke wangu hataishi katika jumba la kifalme la Daudi mfalme wa Israeli, kwa sababu mahali ambapo Sanduku la BWANA limefika ni patakatifu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sulemani akampandisha mke wake binti Farao kutoka Mji wa Daudi na kumleta jumba la kifalme alilokuwa amemjengea, kwa kuwa alisema, “Mke wangu hataishi katika jumba la kifalme la Daudi mfalme wa Israeli, kwa sababu mahali ambapo Sanduku la bwana limefika ni patakatifu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sulemani akamleta binti Farao kutoka mji wa Daudi mpaka nyumba aliyomjengea; kwa kuwa alisema, Mke wangu hatakaa nyumbani mwa Daudi mfalme wa Israeli, kwa kuwa ni patakatifu, mahali palipofika sanduku la BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Solomoni alimhamisha binti Farao mfalme wa Misri, kutoka mji wa Daudi, akampeleka kwenye nyumba aliyomjengea. Alisema, “Mke wangu hataishi katika nyumba ya Daudi mfalme wa Israeli, kwa maana mahali pote ambapo sanduku la Mwenyezi-Mungu limekuwa, ni patakatifu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Binti Farao Salomo akamtoa mjini mwa Dawidi, akampeleka kukaa katika nyumba, aliyomjengea, kwani alisema: Mwanamke asikae kwangu nyumbani mwa Dawidi, mfalme wa Waisiraeli, kwa kuwa ni takatifu, kwani Sanduku la Bwana liliingia mumo humo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sulemani akamleta binti Farao kutoka mji wa Daudi mpaka nyumba aliyomjengea; kwa kuwa alisema, Mke wangu hatakaa nyumbani mwa Daudi mfalme wa Israeli, kwa kuwa ni patakatifu, mahali palipofika sanduku la BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Solomono alimuhamisha binti wa mufalme wa Misri, kutoka muji wa Daudi, akamupeleka kwenye nyumba aliyomujengea. Akasema: “Muke wangu hataishi katika nyumba ya Daudi mufalme wa Israeli, kwa maana pahali pote ambapo sanduku la Yawe limekuwa, ni patakatifu.”