2 Chronicles 8:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huramu alimpelekea merikebu zilizokuwa chini ya uongozi wa maofisa wake, pamoja na mabaharia stadi. Hao, pamoja na maofisa wa Solomoni, walisafiri hadi Ofiri, na kuchukua kutoka huko dhahabu, wakamletea mfalme Solomoni kiasi cha kilo 15,000.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naye Hiramu alimpelekea meli zilizoongozwa na maafisa wake mwenyewe, watu waliokuwa na ujuzi wa baharini. Hawa watu pamoja na wale wa Sulemani wakasafiri kwa bahari hadi Ofiri, wakaleta kutoka huko talanta mia nne na hamsini za dhahabu, ambazo walimkabidhi Mfalme Sulemani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Hiramu akamletea merikebu kwa mikono ya watumishi wake, na watumishi waliokuwa wana-maji; nao wakafika Ofiri pamoja na watumishi wa Sulemani, wakachukua kutoka huko talanta mia nne na hamsini za dhahabu, wakamletea mfalme Sulemani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huramu alimpelekea merikebu zilizokuwa chini ya uongozi wa maofisa wake, pamoja na mabaharia stadi. Hao, pamoja na maofisa wa Solomoni, walisafiri hadi Ofiri, na kuchukua kutoka huko dhahabu, wakamletea mfalme Solomoni kiasi cha kilo 15,000.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naye Hiramu alimpelekea meli zilizoongozwa na maafisa wake mwenyewe, watu ambao walikuwa na ujuzi wa baharini. Hawa watu pamoja na wale wa Solomoni wakasafiri kwa njia ya bahari mpaka Ofiri, wakaleta kutoka huko talanta 450 za dhahabu ambayo walimkabidhi Mfalme Solomoni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naye Hiramu alimpelekea meli zilizoongozwa na maafisa wake mwenyewe, watu waliokuwa na ujuzi wa baharini. Hawa watu pamoja na wale wa Sulemani wakasafiri kwa bahari mpaka Ofiri, wakaleta kutoka huko talanta 450 za dhahabu, ambazo walimkabidhi Mfalme Sulemani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Hiramu akamletea merikebu kwa mikono ya watumishi wake, na watumishi waliokuwa wanamaji; nao wakafika Ofiri pamoja na watumishi wa Sulemani, wakachukua kutoka huko talanta mia nne na hamsini za dhahabu, wakamletea mfalme Sulemani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huramu alimpelekea merikebu zilizokuwa chini ya uongozi wa maofisa wake, pamoja na mabaharia stadi. Hao, pamoja na maofisa wa Solomoni, walisafiri hadi Ofiri, na kuchukua kutoka huko dhahabu, wakamletea mfalme Solomoni kiasi cha kilo 15,000.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huramu akatuma kwake vyombo vilivyopelekwa na watumishi wake pamoja na watumishi walioyajua mambo ya baharini; wakaenda Ofiri pamoja na watumishi wake Salomo, wakachukua huko vipande vya dhahabu 450, ndio frasila 1350, wakampelekea mfalme salomo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Hiramu akamletea merikebu kwa mikono ya watumishi wake, na watumishi waliokuwa wana-maji; nao wakafika Ofiri pamoja na watumishi wa Sulemani, wakachukua kutoka huko talanta mia nne na hamsini za dhahabu, wakamletea mfalme Sulemani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hiramu akamupelekea mashua zilizokuwa chini ya uongozi wa watumishi wake, pamoja na wafundi wa mashua. Wale, pamoja na watumishi wa Solomono, wakasafiri mpaka Ofiri, na kubeba kutoka kule zahabu, wakamuletea mufalme Solomono yapata kilo elfu kumi na tano.