2 Chronicles 8:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
mji wa Baalathi, na miji yake yote ya ghala, magari yake ya kukokotwa na ya wapandafarasi wake, na chochote alichotaka kujenga katika Yerusalemu, Lebanoni au kwingineko katika ufalme wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sulemani pia akajenga Baalathi na miji yake yote ya kuhifadhia vitu, na miji kwa ajili ya magari yake ya vita na kwa ajili ya farasi wake, chochote alichotaka kujenga katika Yerusalemu, katika Lebanoni na katika nchi yote aliyotawala.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na Baalathi, na miji yote ya hazina Sulemani aliyokuwa nayo, na miji yote ya magari yake, na miji ya wapanda farasi wake, na ya anasa yote aliyopenda Sulemani kujenga humo Yerusalemu, na katika Lebanoni, na katika nchi yote ya mamlaka yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
mji wa Baalathi, na miji yake yote ya ghala, magari yake ya kukokotwa na ya wapandafarasi wake, na chochote alichotaka kujenga katika Yerusalemu, Lebanoni au kwingineko katika ufalme wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
pia akajenga Baalathi na miji yake yote ya kuhifadhia vitu na miji yote kwa ajili ya magari yake ya vita na kwa ajili ya farasi wake pamoja na kila alichotaka kukijenga katika Yerusalemu, katika Lebanoni na katika nchi yote aliyotawala.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sulemani pia akajenga Baalathi na miji yake yote ya kuhifadhia vitu, na miji kwa ajili ya magari yake na kwa ajili ya farasi wake, chochote alichotaka kujenga katika Yerusalemu, katika Lebanoni na katika nchi yote aliyotawala.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na Baalathi, na miji yote ya hazina Sulemani aliyokuwa nayo, na miji yote ya magari yake, na miji ya wapanda farasi wake, na ya anasa yote aliyopenda Sulemani kujenga humo Yerusalemu, na katika Lebanoni, na katika nchi yote ya mamlaka yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
mji wa Baalathi, na miji yake yote ya ghala, magari yake ya kukokotwa na ya wapandafarasi wake, na chochote alichotaka kujenga katika Yerusalemu, Lebanoni au kwingineko katika ufalme wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, alivyojenga hata Balati na miji yote yenye vilimbiko, Salomo aliyokuwa nayo, hata miji yote ya magari na miji ya farasi na majengo yote yaliyompendeza Salomo, aliyotaka kuyajenga kwa mapenzi yake mle Yerusalemu nako huko Libanoni na katika nchi yo yote ya ufalme wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na Baalathi, na miji yote ya hazina Sulemani aliyokuwa nayo, na miji yote ya magari yake, na miji ya wapanda farasi wake, na ya anasa yote aliyopenda Sulemani kujenga humo Yerusalemu, na katika Lebanoni, na katika nchi yote ya mamlaka yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
muji wa Balati, na miji yake yote ya kuwekea magari yake ya vita na ya waaskari wapanda-farasi wake, na kitu chochote alichotaka kujenga katika Yerusalema, Lebanoni au nafasi ingine katika ufalme wake.