2 Chronicles 9:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Malkia wa Sheba aliposikia sifa za Solomoni, aliwasili Yerusalemu ili kumjaribu Solomoni kwa maswali magumu. Alifuatana na msafara wa watu, pamoja na ngamia waliobeba manukato, dhahabu nyingi sana na vito vya thamani. Na alipofika kwa Solomoni, alimwuliza maswali yote aliyokuwa nayo moyoni mwake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Malkia wa Sheba aliposikia habari za umaarufu wa Sulemani, akaja Yerusalemu kumjaribu kwa maswali magumu. Alifika akiwa na msafara mkubwa sana, wenye ngamia waliobeba vikolezo, dhahabu nyingi, na vito vya thamani. Alikuja kwa Sulemani na kuzungumza naye mambo yote aliyokuwa nayo moyoni mwake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na malkia wa Sheba aliposikia habari za Sulemani, alikuja ili amjaribu Sulemani kwa maswali ya fumbo huko Yerusalemu, mwenye wafuasi wengi, na ngamia wachukuao manukato, na dhahabu nyingi sana, na vito vya thamani; alipomfikilia Sulemani, akamwambia mambo yote aliyokuwa nayo moyoni mwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Malkia wa Sheba aliposikia sifa za Solomoni, aliwasili Yerusalemu ili kumjaribu Solomoni kwa maswali magumu. Alifuatana na msafara wa watu, pamoja na ngamia waliobeba manukato, dhahabu nyingi sana na vito vya thamani. Na alipofika kwa Solomoni, alimwuliza maswali yote aliyokuwa nayo moyoni mwake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Malkia wa Sheba aliposikia habari za umaarufu wa Solomoni na uhusiano wake na jina la BWANA, huyo malkia akaja kumjaribu kwa maswali magumu. Alipofika Yerusalemu akiwa na msafara mkubwa sana, pamoja na ngamia waliobeba vikolezi, kiasi kikubwa cha dhahabu na vito vya thamani, alikuja kwa Solomoni na kuzungumza naye kuhusu yote ambayo alikuwa nayo moyoni mwake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Malkia wa Sheba aliposikia habari za umaarufu wa Sulemani, huyo malkia akaja Yerusalemu kumjaribu kwa maswali magumu. Alifika akiwa na msafara mkubwa sana, pamoja na ngamia waliobeba vikolezi, kiasi kikubwa cha dhahabu na vito vya thamani, alikuja kwa Sulemani na kuzungumza naye kuhusu yote ambayo alikuwa nayo moyoni mwake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na malkia wa Sheba aliposikia sifa za Sulemani, alikuja ili amjaribu Sulemani kwa maswali ya fumbo huko Yerusalemu, akiwa na wafuasi wengi, na ngamia wachukuao manukato, na dhahabu nyingi sana, na vito vya thamani; alipomfikia Sulemani, akamwambia mambo yote aliyokuwa nayo moyoni mwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Malkia wa Sheba aliposikia sifa za Solomoni, aliwasili Yerusalemu ili kumjaribu Solomoni kwa maswali magumu. Alifuatana na msafara wa watu, pamoja na ngamia waliobeba manukato, dhahabu nyingi sana na vito vya thamani. Na alipofika kwa Solomoni, alimwuliza maswali yote aliyokuwa nayo moyoni mwake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfalme wa kike wa Saba alipousikia uvumi wa Salomo, akaenda Yerusalemu kumjaribu Salomo kwa maulizo ya kufumbafumba, akaja na vikosi vikubwa mno na ngamia waliochukua uvumba na dhahabu nyingi na vito. Alipofika kwa Salomo akasema naye na kumwuliza yote, aliyokuwa nayo moyoni mwake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na malkia wa Sheba aliposikia habari za Sulemani, alikuja ili amjaribu Sulemani kwa maswali ya fumbo huko Yerusalemu, mwenye wafuasi wengi, na ngamia wachukuao manukato, na dhahabu nyingi sana, na vito vya thamani; alipomfikilia Sulemani, akamwambia mambo yote aliyokuwa nayo moyoni mwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Malkia wa Seba aliposikia sifa za Solomono, basi akafika Yerusalema kwa kumujaribu Solomono kwa maulizo magumu. Alifika Yerusalema akisindikizwa na watu wengi sana, pamoja na ngamia waliobeba marasi, zahabu nyingi sana na mawe ya bei kali. Na alipofika kwa Solomono, akamwuliza maulizo yote aliyokuwa nayo ndani ya moyo wake.