2 Chronicles 9:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye mfalme Solomoni alimpatia malkia wa Sheba kila kitu alichotamani, chochote alichoomba mbali na vitu alivyomletea mfalme. Hatimaye malkia aliondoka akarudi katika nchi yake akiwa pamoja na watumishi wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme Sulemani akampa malkia wa Sheba kila kitu alichotamani na kukiomba, zaidi ya vile alivyokuwa amemletea mfalme. Kisha malkia akaondoka na kurudi katika nchi yake, yeye na watumishi wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mfalme Sulemani akampa malkia wa Sheba haja yake yote, kila alilotaka, zaidi ya vile alivyomletea mfalme. Basi akarudi, akaenda zake katika nchi yake, yeye na watumishi wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye mfalme Solomoni alimpatia malkia wa Sheba kila kitu alichotamani, chochote alichoomba mbali na vitu alivyomletea mfalme. Hatimaye malkia aliondoka akarudi katika nchi yake akiwa pamoja na watumishi wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme Solomoni akampa Malkia wa Sheba kila kitu alichohitaji na kukiomba, zaidi ya vile alivyokuwa amemletea mfalme. Kisha malkia akaondoka akarudi kwenye nchi yake mwenyewe pamoja na wafuasi wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme Sulemani akampa Malkia wa Sheba kila kitu alichotamani na kukiomba, zaidi ya vile alivyokuwa amemletea mfalme. Kisha malkia akaondoka na kurudi katika nchi yake, yeye na watumishi wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mfalme Sulemani akampa malkia wa Sheba kila kitu alichokitaka na zaidi ya vile alivyomletea mfalme. Basi akarudi, akaenda zake katika nchi yake, yeye na watumishi wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye mfalme Solomoni alimpatia malkia wa Sheba kila kitu alichotamani, chochote alichoomba mbali na vitu alivyomletea mfalme. Hatimaye malkia aliondoka akarudi katika nchi yake akiwa pamoja na watumishi wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha mfalme Salomo akampa mfalme wa kike wa Saba yote, aliyopendezwa nayo, aliyomwomba, kuliko yale, aliyomletea mfalme; kisha akarudi kwenda kwao katika nchi yake, yeye na watumishi wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mfalme Sulemani akampa malkia wa Sheba haja yake yote, kila alilotaka, zaidi ya vile alivyomletea mfalme. Basi akarudi, akaenda zake katika nchi yake, yeye na watumishi wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye mufalme Solomono alimupatia malkia wa Seba kila kitu alichotamani, kitu chochote alichoomba zaidi ya vitu alivyomuletea mufalme. Kisha malkia akaondoka na kurudi katika inchi yake akiwa pamoja na watumishi wake.