2 Chronicles 9:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Pia alitengeneza ngao ndogondogo 300, kila moja ilipakwa dhahabu ipatayo kilo tatu, halafu mfalme akaziweka katika jengo lililoitwa Nyumba ya Msitu wa Lebanoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akatengeneza pia ngao ndogo mia tatu za dhahabu iliyofuliwa, kila ngao ikiwa na uzito wa mane tatu za dhahabu. Mfalme akaziweka katika Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na vigao mia tatu vya dhahabu iliyofuliwa; kigao kimoja hupata shekeli mia tatu za dhahabu; mfalme akaviweka katika nyumba ya mwitu wa Lebanoni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Pia alitengeneza ngao ndogondogo 300, kila moja ilipakwa dhahabu ipatayo kilo tatu, halafu mfalme akaziweka katika jengo lililoitwa Nyumba ya Msitu wa Lebanoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akatengeneza pia ngao ndogo 300 za dhahabu iliyofuliwa, kila ngao ikiwa ya uzito wa mane tatu za dhahabu. Mfalme akaziweka katika Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akatengeneza pia ngao ndogo 300 za dhahabu iliyofuliwa, kila ngao ikiwa na uzito wa mane tatu za dhahabu. Mfalme akaziweka katika Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na vigao mia tatu vya dhahabu iliyofuliwa; kigao kimoja hupata shekeli mia tatu za dhahabu; mfalme akaviweka katika nyumba ya msitu wa Lebanoni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Pia alitengeneza ngao ndogondogo 300, kila moja ilipakwa dhahabu ipatayo kilo tatu, halafu mfalme akaziweka katika jengo lililoitwa Nyumba ya Msitu wa Lebanoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akatengeneza ngao ndogo 300 za dhahabu zilizofuliwa, hizi ngao ndogo kila moja ikatumiwa sekeli 300, ndio ratli tisa za dhahabu; mfalme akaziweka katika nyumba ya mwituni kwa Libanoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na vigao mia tatu vya dhahabu iliyofuliwa; kigao kimoja hupata shekeli mia tatu za dhahabu; mfalme akaviweka katika nyumba ya mwitu wa Lebanoni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile alitengeneza ngao ndogondogo mia tatu, kila moja ilipakwa zahabu yapata kilo tatu, halafu mufalme akaziweka katika jengo lililoitwa Nyumba ya Pori la Lebanoni.