2 Chronicles 9:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kiti hicho kilikuwa na ngazi sita na kiti cha kuegemea miguu cha dhahabu, vyote hivyo vilikuwa vimeshikamanishwa na kiti hicho cha enzi; na kila upande kilikuwa na mahali pa kuegemeza mikono; pia kilikuwa na sanamu mbili za simba karibu na mahali hapo pa kuegemeza mikono.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kiti hicho kilikuwa na ngazi sita na mahali pa kuwekea miguu vyote vya dhahabu. Kila upande wa kiti ulikuwa na mahali pa kuegemeza mkono, na simba aliyesimama kando kila upande.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kiti kile kilikuwa na daraja sita, tena na kikao cha miguu cha dhahabu, navyo vilikuwa vimeshikamana na kiti; na mikono huko na huko mahali pa kuketi, na simba wawili wakisimama kando ya hiyo mikono.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kiti hicho kilikuwa na ngazi sita na kiti cha kuegemea miguu cha dhahabu, vyote hivyo vilikuwa vimeshikamanishwa na kiti hicho cha enzi; na kila upande kilikuwa na mahali pa kuegemeza mikono; pia kilikuwa na sanamu mbili za simba karibu na mahali hapo pa kuegemeza mikono.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kiti hicho kilikuwa na ngazi sita na mahali pakuwekea miguu vyote vya dhahabu. Upande wa kuume na wa kushoto wa hicho kiti palikuwa na mahali pa kuegemeza mikono, pakiwa na sanamu ya simba iliyosimama kila upande.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kiti hicho kilikuwa na ngazi sita na mahali pa kuwekea miguu vyote vya dhahabu. Pande zote za kiti kulikuwa na mahali pa kuegemeza mikono, na simba wawili wakisimama kando ya hiyo mikono.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kiti kile kilikuwa na ngazi sita, tena na kikao cha miguu cha dhahabu, navyo vilikuwa vimeshikamana na kiti; na kila upande wa kiti hicho palikuwa na pakuegemeza mikono, na simba wawili walisimama kando ya hiyo mikono.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kiti hicho kilikuwa na ngazi sita na kiti cha kuegemea miguu cha dhahabu, vyote hivyo vilikuwa vimeshikamanishwa na kiti hicho cha enzi; na kila upande kilikuwa na mahali pa kuegemeza mikono; pia kilikuwa na sanamu mbili za simba karibu na mahali hapo pa kuegemeza mikono.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hicho kiti cha kifalme kilikuwa na vipago sita vya kukipandia, tena hapo chini yake palikuwa pamefanyizwa pa kuwekea miguu, napo palikuwa pa dhahabu. Tena hapo pa kukalia palikuwa na maegemeo huku na huko, nayo mifano miwili ya simba ilikuwa imesimama hapo penye maegemeo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kiti kile kilikuwa na daraja sita, tena na kikao cha miguu cha dhahabu, navyo vilikuwa vimeshikamana na kiti; na mikono huko na huko mahali pa kuketi, na simba wawili wakisimama kando ya hiyo mikono.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kiti hicho kilikuwa na ngazi sita na kiti cha kuegemea miguu cha zahabu, vyote hivyo vilikuwa vimeshikamanishwa na kiti hicho cha kifalme; na kila upande kilikuwa na pahali pa kuegemeza mikono tena kilikuwa na sanamu mbili za simba karibu na pahali pale pa kuegemeza mikono.