2 Chronicles 9:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Solomoni aliyajibu maswali yote; hapakuwapo na jambo lolote aliloshindwa kumweleza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sulemani alimjibu maswali yake yote, wala hakukuwa na jambo lolote lililokuwa gumu kwake hata asiweze kumwelezea.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Sulemani akamfumbulia maswali yake yote; wala halikuwako neno alilofichiwa Sulemani, asimwambie.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Solomoni aliyajibu maswali yote; hapakuwapo na jambo lolote aliloshindwa kumweleza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Solomoni akamjibu maswali yake yote, wala hakukuwa na jambo lo lote lililokuwa gumu kwa mfalme asiweze kumwelezea.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sulemani akamjibu maswali yake yote, wala hakukuwa na jambo lolote lililokuwa gumu kwake asiweze kumwelezea.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Sulemani akamfumbulia maswali yake yote; wala halikuwako neno aliloficha Sulemani, asimwambie.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Solomoni aliyajibu maswali yote; hapakuwapo na jambo lolote aliloshindwa kumweleza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Salomo akamwelezea yote, aliyomwuliza, halikuwako neno lililofichika maana kwake Salomo, asiloweza kumwelezea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Sulemani akamfumbulia maswali yake yote; wala halikuwako neno alilofichiwa Sulemani, asimwambie.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Solomono akajibu maulizo yote, hakukuwa jambo lolote aliloshindwa kumwelezea.