2 Chronicles 9:20 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Vikombe vyote vya mfalme Solomoni vilikuwa vya dhahabu, na vyombo vyote vilivyokuwa katika Nyumba ya Msitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu safi. Fedha haikuhesabiwa kuwa kitu cha thamani katika siku za Solomoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Vikombe vyote vya Mfalme Sulemani vya kunywea vilikuwa vya dhahabu na vyombo vyote vya nyumbani katika Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu safi. Hakukuwa na kitu kilichotengenezwa kwa fedha, kwa sababu fedha ilionekana ya thamani ndogo wakati wa Sulemani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na vyombo vyote vya kunywea vya mfalme Sulemani vilikuwa vya dhahabu, na vyombo vyote vya nyumba ya mwitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu iliyosafika; fedha haikuhesabiwa kuwa kitu siku za Sulemani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Vikombe vyote vya mfalme Solomoni vilikuwa vya dhahabu, na vyombo vyote vilivyokuwa katika Nyumba ya Msitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu safi. Fedha haikuhesabiwa kuwa kitu cha thamani katika siku za Solomoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Vikombe vyote vya Mfalme Solomoni vya kunywea vilikuwa vya dhahabu na vyombo vyote vya nyumbani katika Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu safi. Hakukuwa na kitu kilichotengenezwa kwa fedha, kwa sababu fedha ilionekana ya thamani ndogo wakati wa Solomoni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Vikombe vyote vya Mfalme Sulemani vya kunywea vilikuwa vya dhahabu na vyombo vyote vya nyumbani katika Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu safi. Hakukuwa na kitu kilichotengenezwa kwa fedha, kwa sababu fedha ilionekana ya thamani ndogo wakati wa Sulemani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na vyombo vyote vya kunywea vya mfalme Sulemani vilikuwa vya dhahabu, na vyombo vyote vya nyumba ya msitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu safi; fedha haikuhesabiwa kuwa kitu siku za Sulemani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Vikombe vyote vya mfalme Solomoni vilikuwa vya dhahabu, na vyombo vyote vilivyokuwa katika Nyumba ya Msitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu safi. Fedha haikuhesabiwa kuwa kitu cha thamani katika siku za Solomoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Navyo vyombo vyote vya kunywea vya mfalme Salomo vilikuwa vya dhahabu, navyo vyombo vyote vya ile nyumba ya mwituni kwa Libanoni vilikuwa vya dhahabu zilizong'azwa; kwani fedha ziliwaziwa kuwa si kitu katika siku za Salomo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na vyombo vyote vya kunywea vya mfalme Sulemani vilikuwa vya dhahabu, na vyombo vyote vya nyumba ya mwitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu iliyosafika; fedha haikuhesabiwa kuwa kitu siku za Sulemani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vikombe vyote vya mufalme Solomono vilikuwa vya zahabu, na vyombo vyote vilivyokuwa katika Nyumba ya Pori ya Lebanoni vilikuwa vya zahabu safi. Feza haikuhesabiwa kuwa kitu cha bei kali katika siku za Solomono.