2 Chronicles 9:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
tena alipotazama chakula kilichoandaliwa mezani pwake na kuona jinsi maofisa wake walivyoketi mezani na huduma ya watumishi wake na jinsi walivyovalia; pia wanyweshaji wake na jinsi walivyovalia, tambiko za kuteketeza ambazo alizitoa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, alipoona hayo yote akashangaa sana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
chakula kilichokuwa mezani pake, jinsi maafisa wake walivyokaa, wahudumu katika majoho yao, wanyweshaji wake na sadaka za kuteketezwa alizotoa katika Hekalu la Mwenyezi Mungu, alipatwa na mshangao mkubwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na vyakula vya mezani mwake, na kikao cha watumishi wake, na usimamizi wao wangoje wake, na mavazi yao; na wanyweshaji wake, na mavazi yao; na daraja yake ya kupandia mpaka nyumba ya Bwana; roho yake ilizimia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
tena alipotazama chakula kilichoandaliwa mezani pwake na kuona jinsi maofisa wake walivyoketi mezani na huduma ya watumishi wake na jinsi walivyovalia; pia wanyweshaji wake na jinsi walivyovalia, tambiko za kuteketeza ambazo alizitoa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, alipoona hayo yote akashangaa sana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
chakula kilichokuwa mezani pake, jinsi maafisa wake walivyokaa, wahudumu katika majoho yao, wanyweshaji wake na sadaka za kuteketezwa Solomoni alizotoa katika Hekalu la BWANA alipatwa na mshangao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
chakula kilichokuwa mezani pake, jinsi maafisa wake walivyokaa, wahudumu katika majoho yao, wanyweshaji wake na sadaka za kuteketezwa alizotoa katika Hekalu la bwana alipatwa na mshangao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na vyakula vya mezani mwake, na kikao cha maofisa wake, na huduma ya watumishi wake na mavazi yao; pia wanyweshaji wake na mavazi yao; na daraja yake ya kupandia mpaka nyumba ya BWANA; roho yake ilizimia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
tena alipotazama chakula kilichoandaliwa mezani pwake na kuona jinsi maofisa wake walivyoketi mezani na huduma ya watumishi wake na jinsi walivyovalia; pia wanyweshaji wake na jinsi walivyovalia, tambiko za kuteketeza ambazo alizitoa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, alipoona hayo yote akashangaa sana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
na vilaji vilivyopo mezani na vikao vya watumwa wake na kazi za watumishi wake na mavazi yao, hata watunza vinywaji wake na mavazi yao na dari, aliyoiweka juu ya Nyumba ya Bwana; ndipo, roho yake ilipozimia,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na vyakula vya mezani mwake, na kikao cha watumishi wake, na usimamizi wao wangoje wake, na mavazi yao; na wanyweshaji wake, na mavazi yao; na daraja yake ya kupandia mpaka nyumba ya BWANA; roho yake ilizimia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
chakula kilichotayarishwa kwenye meza yake, jinsi wakubwa wake walivyokaa kwenye meza, kazi ya watumishi wake na namna walivyovaa, wenye kuleta vinywaji na jinsi walivyovaa, na sadaka za kuteketeza ambazo alitoa katika nyumba ya Yawe.