2 Chronicles 9:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na asifiwe Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ambaye amependezwa nawe, akakuketisha juu ya kiti chake cha enzi, uwe mfalme kwa niaba yake Mwenyezi-Mungu, Mungu wako. Kwa sababu Mungu wako amewapenda Waisraeli na kuwaimarisha milele, amekuweka wewe uwe mfalme juu yao ili udumishe haki na uadilifu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ahimidiwe Mwenyezi Mungu, Mungu wako, ambaye amependezwa sana nawe, na akakuweka kwenye kiti chake cha ufalme utawale kwa niaba ya Mwenyezi Mungu, Mungu wako. Kwa sababu ya upendo wa Mungu wako kwa Israeli na shauku yake ya kuwathibitisha milele, amekufanya wewe mfalme juu yao, ili kudumisha haki na uadilifu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na ahimidiwe Bwana, Mungu wako, aliyependezwa nawe, ili akuweke juu ya kiti chake cha enzi, kuwa mfalme wake Bwana, Mungu wako; kwa kuwa Mungu wako amewapenda Israeli, kuwathibitisha milele, kwa hiyo amekufanya kuwa mfalme juu yao, ufanye hukumu na haki.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na asifiwe Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ambaye amependezwa nawe, akakuketisha juu ya kiti chake cha enzi, uwe mfalme kwa niaba yake Mwenyezi-Mungu, Mungu wako. Kwa sababu Mungu wako amewapenda Waisraeli na kuwaimarisha milele, amekuweka wewe uwe mfalme juu yao ili udumishe haki na uadilifu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ahimidiwe BWANA Mungu wako, ambaye amependezwa sana nawe na kukuweka juu ya kiti chake cha ufalme kutawala kwa niaba ya BWANA Mungu wako. Kwa sababu ya upendo wa Mungu wako kwa Israeli na shauku yake ya kuwadhibitisha milele, amekufanya wewe mfalme juu yao, ili kudumisha haki na uadilifu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ahimidiwe bwana Mwenyezi Mungu wako, ambaye amependezwa sana nawe, na akakuweka juu ya kiti chake cha ufalme utawale kwa niaba ya bwana Mwenyezi Mungu wako. Kwa sababu ya upendo wa Mungu wako kwa Israeli na shauku yake ya kuwadhibitisha milele, amekufanya wewe mfalme juu yao, ili kudumisha haki na uadilifu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na ahimidiwe BWANA, Mungu wako, aliyependezwa nawe, ili akuweke juu ya kiti chake cha enzi, kuwa mfalme wake BWANA, Mungu wako; kwa kuwa Mungu wako amewapenda Israeli, kuwathibitisha milele, kwa hiyo amekufanya kuwa mfalme juu yao, ufanye hukumu na haki.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na asifiwe Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ambaye amependezwa nawe, akakuketisha juu ya kiti chake cha enzi, uwe mfalme kwa niaba yake Mwenyezi-Mungu, Mungu wako. Kwa sababu Mungu wako amewapenda Waisraeli na kuwaimarisha milele, amekuweka wewe uwe mfalme juu yao ili udumishe haki na uadilifu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana Mungu wako na atukuzwe, kwa kuwa alipendezwa na wewe, akakukalisha katika kiti chake cha kifalme, uwe mfalme wa Bwana Mungu wako! Kwa kuwa Mungu wako anawapenda Waisiraeli, awapatie kuwapo kale na kale, alikupa kuwa mfalme wao, uwaamue kwa wongofu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na ahimidiwe BWANA, Mungu wako, aliyependezwa nawe, ili akuweke juu ya kiti chake cha enzi, kuwa mfalme wake BWANA, Mungu wako; kwa kuwa Mungu wako amewapenda Israeli, kuwathibitisha milele, kwa hiyo amekufanya kuwa mfalme juu yao, ufanye hukumu na haki.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na asifiwe Yawe, Mungu wako, ambaye amependezwa nawe, akakuikalisha juu ya kiti chake cha kifalme, ukuwe mufalme kwa jina la Yawe, Mungu wako. Kwa sababu Mungu wako amewapenda Waisraeli na kuwaimarisha milele, amekuweka wewe ukuwe mufalme juu yao kusudi uimarishe uhaki na sheria ya Mungu.”