2 Corinthians 1:15 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nikiwa na matumaini hayo, nilikusudia kuja kwenu hapo awali ili mpate baraka maradufu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa nilikuwa na uhakika wa mambo haya, nilitaka nije kwenu kwanza, ili mpate faida mara mbili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nikiwa na tumaini hilo nalitaka kufika kwenu hapo kwanza, ili mpate karama ya pili;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nilikuwa na uhakika sana juu ya haya yote. Ndiyo maana niliweka mpango wa kuwatembelea kwanza. Kisha mngebarakikwa mara mbili.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nikiwa na matumaini hayo, nilikusudia kuja kwenu hapo awali ili mpate baraka maradufu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nikiwa na matumaini hayo, nilikusudia kuja kwenu hapo awali ili mpate baraka maradufu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa nilikuwa na uhakika wa mambo haya, nilitaka nije kwenu kwanza, ili mpate faida mara mbili.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa nilikuwa na uhakika wa mambo haya, nilitaka nije kwenu kwanza, ili mpate faida mara mbili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nikiwa na tumaini hilo nilitaka kufika kwenu hapo kwanza, ili mpate karama ya pili;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nikiwa na matumaini hayo, nilikusudia kuja kwenu hapo awali ili mpate baraka maradufu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa kushikizwa hivyo moyoni, nalitaka kufika kwenu hapo kwanza, ninyi mpate kuamkiwa mara mbili:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nikiwa na tumaini hilo nalitaka kufika kwenu hapo kwanza, ili mpate karama ya pili;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika tumaini hili nilikusudia kufika kwenu kwanza kusudi mupate furaha mara mbili.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na nikiwa na timiaini hilo nalitaka kwenda kwenu hapo kwanza, illi mpate karama ya pili;