2 Corinthians 1:18 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu ni ukweli tupu; basi, kile tulichowaambia nyinyi si jambo la “Ndiyo” na “Siyo”.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hakika kama Mungu alivyo mwaminifu, maneno yetu kwenu hayajakuwa “Ndiyo” na “Siyo”.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini kama Mungu alivyo mwaminifu, neno letu kwenu si Ndiyo na siyo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kama ambavyo kwa hakika mnaweza kumwamini Mungu, basi mnaweza kuamini kuwa lile tunalowaambia kamwe haliwezi kuwa ndiyo na hapana kwa pamoja.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mungu ni ukweli mtupu; basi, kile tulichowaambia ninyi si jambo la “Ndiyo” na “Siyo”.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu ni ukweli tupu; basi, kile tulichowaambia nyinyi si jambo la “Ndiyo” na “Siyo”.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hakika kama Mungu alivyo mwaminifu, maneno yetu kwenu hayajawa “Ndiyo na Siyo.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hakika kama Mungu alivyo mwaminifu, maneno yetu kwenu hayajawa “Ndiyo na Siyo.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini kama Mungu alivyo mwaminifu, neno letu kwenu si Ndiyo na Siyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu ni ukweli tupu; basi, kile tulichowaambia nyinyi si jambo la “Ndiyo” na “Siyo”.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Mungu ni mwelekevu, amejua ya kuwa: Neno letu, tulilowaambia, halina maana mbili: kuitikia na kukataa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini kama Mungu alivyo mwaminifu, neno letu kwenu si Ndiyo na siyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama vile Mungu anavyokuwa mwaminifu, hakika mambo tuliyowaambia hayakukuwa ya kusema “Ndiyo” na “Hapana” kwa mara moja.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini kama Mungu alivyo mwaminifu, neno letu kwenu halikuwa ndiyo na siyo.