2 Corinthians 1:19 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana Kristo Yesu, Mwana wa Mungu, ambaye mimi, Silwano na Timotheo, tulimhubiri kwenu, hakuwa mtu wa “Ndiyo” na “Siyo;” bali yeye daima ni “Ndiyo” ya Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa Isa Al-Masihi, Mwana wa Mungu, ambaye mimi, Silvano, na Timotheo tulimhubiri kwenu, hakuwa “Ndiyo” na “Siyo”, bali kwake yeye siku zote ni “Ndiyo”.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana Mwana wa Mungu, Kristo Yesu, aliyehubiriwa katikati yenu na sisi, yaani, mimi na Silwano na Timotheo, hakuwa Ndiyo na siyo; bali katika yeye ni Ndiyo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mwana wa Mungu, Yesu Kristo, Yeye ambaye Sila, Timotheo, na mimi tuliwaeleza habari zake, hakutokea kuwa ni ndiyo na hapana kwa ahadi za Mungu. Kinyume chake ndiyo ya Mungu imethibitika daima katika Kristo kuwa ni ndiyo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana Kristo Yesu, Mwana wa Mungu, ambaye mimi, Silwano na Timotheo, tulimhubiri kwenu, hakuwa mtu wa “Ndiyo” na “Siyo”; bali yeye daima ni “Ndiyo” ya Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana Kristo Yesu, Mwana wa Mungu, ambaye mimi, Silwano na Timotheo, tulimhubiri kwenu, hakuwa mtu wa “Ndiyo” na “Siyo;” bali yeye daima ni “Ndiyo” ya Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, ambaye tulimhubiri kwenu: Mimi, Silvano na Timotheo, hakuwa “Ndiyo” na “Siyo,” bali katika yeye siku zote ni “Ndiyo.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa Isa Al-Masihi, Mwana wa Mungu, ambaye tulimhubiri kwenu: Mimi, Silvano na Timotheo, hakuwa “Ndiyo” na “Siyo,” bali kwake yeye siku zote ni “Ndiyo.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana Mwana wa Mungu, Kristo Yesu, aliyehubiriwa katikati yenu na sisi, yaani, mimi na Silwano na Timotheo, hakuwa Ndiyo na Siyo; bali katika yeye ni Ndiyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana Kristo Yesu, Mwana wa Mungu, ambaye mimi, Silwano na Timotheo, tulimhubiri kwenu, hakuwa mtu wa “Ndiyo” na “Siyo;” bali yeye daima ni “Ndiyo” ya Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani Kristo Yesu, Mwana wa Mungu, aliyetangazwa kwenu na sisi, mimi na Silwano na Timoteo, hakuwa mwenye kuitikia na kukataa, ila mwake yeye mlikuwa kuitikia tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana Mwana wa Mungu, Kristo Yesu, aliyehubiriwa katikati yenu na sisi, yaani, mimi na Silwano na Timotheo, hakuwa Ndiyo na siyo; bali katika yeye ni Ndiyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana Yesu Kristo, Mwana wa Mungu ambaye Silvano, Timoteo na mimi mwenyewe tuliyemuhubiri kwenu hakukuja kusema “Ndiyo” na “Hapana.” Lakini yeye ni “Ndiyo” inayotoka kwa Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana Mwana wa Mungu, Yesu Kristo, aliyekhubiriwa na sisi kati yenu, na mimi na Silwano na Timotheo, hakuwa ndiyo na siyo; bali katika yeye ndiyo imepata kuwako.