2 Corinthians 1:20 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana ndani yake ahadi zote za Mungu zimekuwa “Ndiyo”. Kwa sababu hiyo, “Amina” yetu husemwa kwa njia ya Kristo kwa ajili ya kumtukuza Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana ahadi zote za Mungu zilizo katika Al-Masihi ni “Ndiyo”. Kwa sababu hii, ni kwake yeye tunasema “Amen” kwa utukufu wa Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni Ndiyo; tena kwa hiyo katika yeye ni Amin; Mungu apate kutukuzwa kwa sisi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndiyo kwa ahadi zote za Mungu katika Kristo. Na hii ndiyo maana twasema “Amina” Katika Kristo kwa utukufu wa Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana ndani yake ahadi zote za Mungu zimekuwa “Ndiyo”. Kwa sababu hiyo, “Amina” yetu husemwa kwa njia ya Kristo kwa ajili ya kumtukuza Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana ndani yake ahadi zote za Mungu zimekuwa “Ndiyo”. Kwa sababu hiyo, “Amina” yetu husemwa kwa njia ya Kristo kwa ajili ya kumtukuza Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana ahadi zote za Mungu zilizo katika Kristo ni “Ndiyo.” Kwa sababu hii ni katika yeye tunasema “Amen” kwa utukufu wa Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana ahadi zote za Mungu zilizo katika Al-Masihi ni “Ndiyo.” Kwa sababu hii ni kwake yeye tunasema “Amen” kwa utukufu wa Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni Ndiyo; tena kwa hiyo katika yeye ni Amin; Mungu apate kutukuzwa kwa sisi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana ndani yake ahadi zote za Mungu zimekuwa “Ndiyo”. Kwa sababu hiyo, “Amina” yetu husemwa kwa njia ya Kristo kwa ajili ya kumtukuza Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani viagio vyote vya Mungu vilivyoko vimeitikiwa naye, kisha vimetimizwa naye, Mungu apate kutukuzwa nasi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni Ndiyo; tena kwa hiyo katika yeye ni Amin; Mungu apate kutukuzwa kwa sisi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana yeye ndiye anayetimiza ahadi zote za Mungu. Vilevile ni kwa njia ya Yesu Kristo tunasema “Amina” kwa kumutukuza Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni ndiyo; na katika yeye ni Amin, Mungu apate kutukuzwa kwa kazi yetu.