2 Corinthians 1:23 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu ndiye shahidi wangu; yeye anajua moyo wangu! Mimi sikuja tena Korintho kwa sababu tu ya kuwahurumieni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Namwita Mungu awe shahidi wangu kwamba sikurudi Korintho kwa sababu niliwahurumia ninyi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini mimi namwita Mungu awe shahidi juu ya roho yangu, ya kwamba, kwa kuwahurumia sijafika Korintho.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninawaambia hili, na ninamwomba Mungu awe shahidi wangu kuwa ni la kweli: Sababu iliyonifanya nisirudi tena Korintho ni kuwa nilitaka niepuke kuwapa karipio lenye nguvu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mungu ndiye shahidi wangu—yeye anajua moyo wangu! Mimi sikuja tena Korintho, kwa sababu tu ya kuwahurumieni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu ndiye shahidi wangu; yeye anajua moyo wangu! Mimi sikuja tena Korintho kwa sababu tu ya kuwahurumieni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mungu ni shahidi wangu kwamba ilikuwa ni kwa ajili ya kuwahurumia ninyi sikurudi Korintho.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mungu ni shahidi wangu kwamba ilikuwa ni kwa ajili ya kuwahurumia ninyi sikurudi Korintho.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini mimi namwita Mungu awe shahidi juu ya roho yangu, ya kwamba, kwa kuwahurumia sijafika Korintho.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu ndiye shahidi wangu; yeye anajua moyo wangu! Mimi sikuja tena Korintho kwa sababu tu ya kuwahurumieni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mimi namtaja Mungu, aushuhudie moyo wangu ya kuwa: Sujaja tena Korinto, nipate kuwajia mwenye upole.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini mimi namwita Mungu awe shahidi juu ya roho yangu, ya kwamba, kwa kuwahurumia sijafika Korintho.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninamutaja Mungu kuwa mushuhuda wangu, yeye anajua roho yangu! Mimi nilikusudia kutorudia tena Korinto kwa sababu ya kuwasikilia huruma.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini mimi namwitia Mungu awe shahidi juu ya roho yangu, ya kwamba, kwa kuwahurumia sijaenda Korintho.