2 Corinthians 1:6 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ikiwa tunapata taabu, basi ni kwa ajili ya faraja na wokovu wenu. Tukifarijika, ni kwa ajili ya kuwafariji nyinyi na kuwaunga mkono mpate nguvu ya kustahimili mateso yaleyale tunayoteseka sisi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ikiwa tunataabika, ni kwa ajili ya faraja na wokovu wenu; tukifarijiwa, ni kwa ajili ya faraja yenu, iwaleteayo saburi ya mateso yale yale yanayotupata.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini ikiwa sisi tu katika dhiki, ni kwa ajili ya faraja yenu na wokovu wenu; au ikiwa twafarijiwa, ni kwa ajili ya faraja yenu; ambayo hutenda kazi yake kwa kustahimili mateso yale yale tuteswayo na sisi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ikiwa tuko katika mateso, tuko kwa ajili ya faraja yenu na wokovu wenu. Na ikiwa tunafarijika, ni kwa sababu tuweze kuwafariji ninyi. Hili huwasaidia katika kuyakubali mateso yale yale tunayopata kwa uvumilivu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ikiwa tunapata taabu, basi ni kwa ajili ya faraja na wokovu wenu. Tukifarijika, ni kwa ajili ya kuwafariji ninyi na kuwaunga mkono mpate nguvu ya kustahimili mateso yaleyale tunayoteseka sisi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ikiwa tunapata taabu, basi ni kwa ajili ya faraja na wokovu wenu. Tukifarijika, ni kwa ajili ya kuwafariji nyinyi na kuwaunga mkono mpate nguvu ya kustahimili mateso yaleyale tunayoteseka sisi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama tunataabika, ni kwa ajili ya faraja na wokovu wenu, kama tukifarijiwa, ni kwa ajili ya faraja yenu, iwaleteayo saburi ya mateso yale yale yanayotupata.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama tunataabika, ni kwa ajili ya faraja na wokovu wenu; kama tukifarijiwa, ni kwa ajili ya faraja yenu, iwaleteayo saburi ya mateso yale yale yanayotupata.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini ikiwa sisi tu katika dhiki, ni kwa ajili ya faraja yenu na wokovu wenu; au ikiwa twafarijiwa, ni kwa ajili ya faraja yenu; ambayo hutenda kazi yake kwa kustahimili mateso yale yale tuteswayo na sisi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ikiwa tunapata taabu, basi ni kwa ajili ya faraja na wokovu wenu. Tukifarijika, ni kwa ajili ya kuwafariji nyinyi na kuwaunga mkono mpate nguvu ya kustahimili mateso yaleyale tunayoteseka sisi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikiwa tunaumizwa, ni kwa kwamba: Ninyi mpate kupozwa mioyo na kuokoka; ikiwa tunapozwa mioyo, ni kwa kwamba: Ninyi mpozwe mioyo, mwipate ile nguvu inayoonekana hapo, mnapoyavumilia mateso yaleyale, tunayoteswa nasi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini ikiwa sisi tu katika dhiki, ni kwa ajili ya faraja yenu na wokovu wenu; au ikiwa twafarijiwa, ni kwa ajili ya faraja yenu; ambayo hutenda kazi yake kwa kustahimili mateso yale yale tuteswayo na sisi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama sisi tunapata taabu ni kusudi mupate kufarijiwa na kuokolewa. Kama tunafarijiwa ninyi vilevile munafarijiwa na kupata nguvu ya kuwawezesha kuvumilia taabu ile ile tunayopata.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini ikiwa sisi tu katika shidda, ni kwa ajili ya faraja yenu na wokofu wenu, ufanyao kazi yake kwa kuvumilia mateso yale yale tuteswayo na sisi: au ikiwa twafarijiwa, ni kwa ajili ya faraja yenu na wokofu wenu.