2 Corinthians 1:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena, matumaini tuliyo nayo kwa ajili yenu ni imara; tunajua kwamba mkishiriki mateso yetu, mtashiriki pia faraja yetu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nalo tumaini letu kwenu ni thabiti, kwa sababu tunajua kwamba kama vile mnavyoshiriki mateso yetu, ndivyo pia mnavyoshiriki faraja yetu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na tumaini letu kwa ajili yenu ni imara, tukijua ya kuwa kama vile mlivyo washiriki wa yale mateso, vivyo hivyo mmekuwa washiriki wa zile faraja.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tumaini letu kwenu liko imara. Tunafahamu kuwa mnashiriki katika mateso yetu. Hivyo tunafahamu pia kuwa mnashiriki katika faraja yetu pia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Tena, matumaini tuliyo nayo kwa ajili yenu ni imara; tunajua kwamba mkishiriki mateso yetu, mtashiriki pia faraja yetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena, matumaini tuliyo nayo kwa ajili yenu ni imara; tunajua kwamba mkishiriki mateso yetu, mtashiriki pia faraja yetu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nalo tumaini letu kwenu ni thabiti, kwa sababu tunajua kwamba kama vile mnavyoshiriki mateso yetu, ndivyo pia mnavyoshiriki katika faraja yetu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nalo tumaini letu kwenu ni thabiti, kwa sababu tunajua kwamba kama vile mnavyoshiriki mateso yetu, ndivyo pia mnavyoshiriki katika faraja yetu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na tumaini letu kwa ajili yenu ni imara, tukijua ya kuwa kama vile mlivyo washiriki wa yale mateso, vivyo hivyo mmekuwa washiriki wa zile faraja.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena, matumaini tuliyo nayo kwa ajili yenu ni imara; tunajua kwamba mkishiriki mateso yetu, mtashiriki pia faraja yetu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Navyo, tunavyongojea kwa ajili yenu, vina nguvu, kwani tumejua: kama mlivyogawiwa mateso, vivyo hivyo mtagawiwa nao upozi wa mioyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na tumaini letu kwa ajili yenu ni imara, tukijua ya kuwa kama vile mlivyo washiriki wa yale mateso, vivyo hivyo mmekuwa washiriki wa zile faraja.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hivi, hatuwezi kukata tumaini tunalokuwa nalo kwenu, kwa maana tunajua kwamba kwa kuwa munashiriki katika taabu yetu, munashiriki vilevile katika kufarijiwa kwetu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na tumaini letu kwa ajili yenu ni imara, tukijua ya kuwa vile vile kama mlivyo washiriki wa yale mateso, vivyo hivyo m washiriki wa zile faraja.