2 Corinthians 1:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndugu, tunataka kuwajulisheni taabu zilizotupata kule Asia; taabu hizo zilitulemea kupita kiasi, hata tukakata matumaini yote ya kuendelea kuishi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndugu wapendwa, hatutaki mkose kujua kuhusu zile taabu tulizopata huko jimbo la Asia. Kwa maana tulilemewa na mizigo sana, kiasi cha kushindwa kuvumilia, hata tulikata tamaa ya kuishi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana ndugu, hatupendi, msijue habari ya dhiki ile iliyotupata katika Asia, ya kwamba tulilemewa mno kuliko nguvu zetu, hata tukakata tamaa ya kuishi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndugu zangu, tunapenda mfahamu juu ya mateso tuliyoyapata hapa Asia. Tulikuwa na mzigo sana huko, ulikuwa mzito kuliko hata nguvu zetu. Hata tulipoteza tumaini la kuishi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ndugu, tunataka kuwajulisheni taabu zilizotupata kule Asia; taabu hizo zilitulemea kupita kiasi, hata tukakata matumaini yote ya kuendelea kuishi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndugu, tunataka kuwajulisheni taabu zilizotupata kule Asia; taabu hizo zilitulemea kupita kiasi, hata tukakata matumaini yote ya kuendelea kuishi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndugu wapendwa, hatutaki msijue kuhusu zile taabu tulizopata huko Asia. Kwa maana tulilemewa na mizigo sana kiasi cha kushindwa kuvumilia, hata tulikata tamaa ya kuishi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndugu wapendwa, hatutaki mkose kujua kuhusu zile taabu tulizopata huko Asia. Kwa maana tulilemewa na mizigo sana, kiasi cha kushindwa kuvumilia, hata tulikata tamaa ya kuishi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana ndugu, hatupendi, msijue habari ya dhiki ile iliyotupata katika Asia, ya kwamba tulilemewa mno kuliko nguvu zetu, hata tukakata tamaa ya kuishi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndugu, tunataka kuwajulisheni taabu zilizotupata kule Asia; taabu hizo zilitulemea kupita kiasi, hata tukakata matumaini yote ya kuendelea kuishi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani hatutaki, ndugu, mkose kuyajua mambo ya maumivu yetu yaliyotupata huko Asia, ya kuwa tulilemewa nayo, yakituumiza kuzipita nguvu zetu, tukapotelewa kwamba: Hatutapona.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana ndugu, hatupendi, msijue habari ya dhiki ile iliyotupata katika Asia, ya kwamba tulilemewa mno kuliko nguvu zetu, hata tukakata tamaa ya kuishi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wandugu, tunataka mujue taabu tuliyopata katika jimbo la Azia. Taabu ile ilitulemea sana hata tukakata tumaini lote la kuendelea kuishi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana hatupendi, ndugu, msijue khabari ya shidda ile iliyotupata katika Asia, ya kwamba tulilemewa mno kuliko nguvu zetu, hatta tukakata tamaa ya kuishi.