2 Corinthians 10:16 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo tutaweza kuihubiri Habari Njema katika nchi nyingine, mbali nanyi; na haitakuwa shauri la kujivunia kazi waliyofanya watu wengine mahali pengine.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
ili tuweze kuhubiri Injili sehemu zilizo mbali na maeneo yenu. Kwa maana hatutaki kujisifu kwa ajili ya kazi ambayo imekwisha kufanyika tayari katika eneo la mtu mwingine.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
hata kuihubiri Injili katika nchi zilizo mbele kupita nchi zenu; tusijisifu katika kipimo cha mtu mwingine kwa mambo yaliyokwisha kutengenezwa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tunataka kuieneza habari njema katika maeneo ya mbali zaidi kupita mji wenu. Hatutaki kujisifia juu ya kazi ambayo imefanywa na mtu mwingine katika eneo lake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hapo tutaweza kuihubiri Habari Njema katika nchi nyingine, mbali nanyi; na haitakuwa shauri la kujivunia kazi waliyofanya watu wengine mahali pengine.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo tutaweza kuihubiri Habari Njema katika nchi nyingine, mbali nanyi; na haitakuwa shauri la kujivunia kazi waliyofanya watu wengine mahali pengine.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
ili tuweze kuhubiri Injili sehemu zilizo mbali na maeneo yenu. Kwa maana hatutaki kujisifu kwa ajili ya kazi ambayo imekwisha kufanyika tayari katika eneo la mtu mwingine.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
ili tuweze kuhubiri Injili sehemu zilizo mbali na maeneo yenu. Kwa maana hatutaki kujisifu kwa ajili ya kazi ambayo imekwisha kufanyika tayari katika eneo la mtu mwingine.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
hata kuihubiri Injili katika nchi zilizo mbele kupita nchi zenu; tusijisifu katika kipimo cha mtu mwingine kwa mambo yaliyokwisha kutengenezwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo tutaweza kuihubiri Habari Njema katika nchi nyingine, mbali nanyi; na haitakuwa shauri la kujivunia kazi waliyofanya watu wengine mahali pengine.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
tupate kuutangaza Utume mwema hata kwao wakaao mbali kuwapita ninyi. Lakini hatutafuti majivuno tukiingia nchi iliyoisha kupigiwa hiyo mbiu njema na wengine.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
hata kuihubiri Injili katika nchi zilizo mbele kupita nchi zenu; tusijisifu katika kipimo cha mtu mwingine kwa mambo yaliyokwisha kutengenezwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha tutaweza kuhubiri Habari Njema katika inchi zinazokuwa mbali kupita inchi yenu, kuliko kujisifu juu ya kazi watu wengine waliyokwisha kufanya kufuatana na kipimo walichopewa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
na kupata ziada hatta kuikhuhiri Injili katika inchi zilizo mpaka mmoja na inchi zenu; tusijisifu katika cheo cha mtu mwingine kwa mambo yaliyokwisha kutengenezwa.