2 Corinthians 10:2 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nawaombeni msinisababishe kuwa mkali wakati nitakapokuja, maana nina hakika naweza kuwa mkali kwa wote wale wanaotudhania kwamba tunaishi kidunia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nawaomba nitakapokuja kwenu nisipaswe kuwa na ujasiri dhidi ya watu fulani kama ninavyotazamia kwa wale wanaodhani kwamba tunaishi kwa kufuata mtazamo wa ulimwengu huu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
naam, naomba kwamba nikiwapo, nisiwe na ujasiri kwa uthabiti ambao nahesabu kuwa nao juu ya wale wanaodhania ya kuwa sisi tunaenenda kwa jinsi ya mwili.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wanadhani sababu ya kutenda yale tunayoyafanya ni kama zile za kidunia. Ninapanga kuwa jasiri sana kinyume chao watu hao hapo ninapokuja kwenu. Tafadhali ninawaomba, sitahitaji kutumia ujasiri huo kwenu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nawaombeni msinisababishe kuwa mkali wakati nitakapokuja, maana nina hakika naweza kuwa mkali kwa wote wale wanaotudhania kwamba tunaishi kidunia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nawaombeni msinisababishe kuwa mkali wakati nitakapokuja, maana nina hakika naweza kuwa mkali kwa wote wale wanaotudhania kwamba tunaishi kidunia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nawaomba nitakapokuja kwenu nisiwe na ujasiri dhidi ya watu fulani, kama ninavyotazamia kwa wale wanaodhani kwamba tunaishi kwa kufuata namna ya ulimwengu huu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nawaomba nitakapokuja kwenu nisiwe na ujasiri dhidi ya watu fulani, kama ninavyotazamia kwa wale wanaodhani kwamba tunaishi kwa kufuata namna ya ulimwengu huu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
naam, naomba kwamba nikiwapo, nisiwe na ujasiri kwa uthabiti ambao nahesabu kuwa nao juu ya wale wanaodhania ya kuwa sisi tunaenenda kwa jinsi ya mwili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nawaombeni msinisababishe kuwa mkali wakati nitakapokuja, maana nina hakika naweza kuwa mkali kwa wote wale wanaotudhania kwamba tunaishi kidunia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nawaomba, msinishurutishe kuyatumia hayo makali nitakapofika. Mwenyewe nadhani, yafaa kuwaendea na nguvu wale wachache wanaotudhania, ya kwamba sisi huendelea na kufuata tamaa za miili.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
naam, naomba kwamba nikiwapo, nisiwe na ujasiri kwa uthabiti ambao nahesabu kuwa nao juu ya wale wanaodhania ya kuwa sisi tunaenenda kwa jinsi ya mwili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninawasihi kwamba nitakapofika kwenu, musinisukume kuwa mukali. Kwa maana nina uhakika kwamba nitawatendea vile wale watu wote wanaozania kwamba sisi tunaishi maisha ya kimwili.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
naam, naomba kwamba nikiwapo, nisiwe na ujasiri kwa uthabiti ambao nahesabu kuwa nao juu ya wale wanaodhani ya kuwasisi tunaenenda kwa jinsi ya mwili.