2 Corinthians 10:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nyinyi hutazama mambo kwa nje tu. Je, yupo mtu yeyote anayedhani kwamba yeye ni wa Kristo? Sawa! Basi, afikirie vilevile kwamba sisi pia ni wa Kristo kama yeye alivyo wa Kristo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mnayaangalia yaliyo mbele ya macho yenu tu. Kama mtu yeyote anaamini kuwa yeye ni mali ya Al-Masihi, basi kumbuka kuwa kama ulivyo wa Al-Masihi, vivyo hivyo na sisi ndivyo tulivyo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yaangalieni yaliyo mbele ya macho yenu. Mtu akijitumainia mwenyewe ya kuwa ni mtu wa Kristo, na afikiri hivi pia nafsini mwake, ya kwamba kama yeye alivyo mtu wa Kristo, vivyo hivyo na sisi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mnatakiwa kuchunguza ukweli halisi wa mambo ulio mbele ya macho yenu. Ikiwa mna uhakika kuwa ninyi ni wa Kristo, mnapaswa kukumbuka kuwa na sisi ni wa Kristo kama ninyi mlivyo wa Kristo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ninyi hutazama mambo kwa nje tu. Je, yupo mtu yeyote anayedhani kwamba yeye ni wa Kristo? Sawa! Basi, afikirie vilevile kwamba sisi pia ni wa Kristo kama yeye alivyo wa Kristo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nyinyi hutazama mambo kwa nje tu. Je, yupo mtu yeyote anayedhani kwamba yeye ni wa Kristo? Sawa! Basi, afikirie vilevile kwamba sisi pia ni wa Kristo kama yeye alivyo wa Kristo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Angalieni yale yaliyo machoni penu. Kama mtu ye yote anaamini kuwa yeye ni mali ya Kristo, basi kumbuka kuwa kama ulivyo wa Kristo, vivyo hivyo na sisi ndivyo tulivyo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Angalieni yale yaliyo machoni penu. Kama mtu yeyote anaamini kuwa yeye ni mali ya Al-Masihi, basi kumbuka kuwa kama ulivyo wa Al-Masihi, vivyo hivyo na sisi ndivyo tulivyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yaangalieni yaliyo mbele ya macho yenu. Mtu akijitumainia mwenyewe ya kuwa ni mtu wa Kristo, na afikiri hivi pia nafsini mwake, ya kwamba kama yeye alivyo mtu wa Kristo, vivyo hivyo ndivyo sisi nasi tulivyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nyinyi hutazama mambo kwa nje tu. Je, yupo mtu yeyote anayedhani kwamba yeye ni wa Kristo? Sawa! Basi, afikirie vilevile kwamba sisi pia ni wa Kristo kama yeye alivyo wa Kristo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yatazameni yanayoonekana machoni! Mtu akijishikiza kwa kwamba: Ni wa Kristo, na atie hili nalo moyoni la kwamba: Kama yeye alivyo wa Kristo, vivyo hivyo nasi!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yaangalieni yaliyo mbele ya macho yenu. Mtu akijitumainia mwenyewe ya kuwa ni mtu wa Kristo, na afikiri hivi pia nafsini mwake, ya kwamba kama yeye alivyo mtu wa Kristo, vivyo hivyo na sisi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninyi munaangalia tu namna vitu vinavyoonekana kwa inje. Mutu yeyote anayejiaminia kwamba yeye ni wa Kristo, inafaa afikiri tena yeye mwenyewe mambo haya: ikiwa yeye ni wa Kristo sisi vilevile ni wa Kristo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Je! mnayaangalia yaliyo mbele ya macho yenu? Mtu akijitumainia nafsi yake ya kuwa yeye ni mtu wa Kristo, na afikiri hivi pia nafsini mwake, ya kwamba kama yeye alivyo mtu wa Kristo, vivyo hivyo na sisi tu watu wa Kristo.