2 Corinthians 11:15 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo si jambo la kushangaza ikiwa na hao watumishi wake wanajisingizia kuwa watumishi wa haki. Mwisho wao watapata kile wanachostahili kufuatana na matendo yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo basi si ajabu kama watumishi wa Shetani nao hujigeuza ili waonekane kama watumishi wa haki. Mwisho wao utakuwa sawa na matendo yao yanavyostahili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo, hiyo haitufanyi sisi kustaajabu ikiwa watumishi wa shetani watajigeuza na kujifanya kuwa watumishi wanaofanya yaliyo ya haki. Lakini mwishowe watapokea hukumu wanayostahili.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa hiyo si jambo la kushangaza ikiwa na hao watumishi wake wanajisingizia kuwa watumishi wa haki. Mwisho wao watapata kile wanachostahili kufuatana na matendo yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo si jambo la kushangaza ikiwa na hao watumishi wake wanajisingizia kuwa watumishi wa haki. Mwisho wao watapata kile wanachostahili kufuatana na matendo yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo basi si ajabu, kama watumishi wa Shetani nao hujigeuza ili waonekane kama watumishi wa haki. Mwisho wao utakuwa sawa na matendo yao yanavyostahili.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo basi si ajabu, kama watumishi wa Shetani nao hujigeuza ili waonekane kama watumishi wa haki. Mwisho wao utakuwa sawa na matendo yao yanavyostahili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo si jambo la kushangaza ikiwa na hao watumishi wake wanajisingizia kuwa watumishi wa haki. Mwisho wao watapata kile wanachostahili kufuatana na matendo yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo si neno kubwa, watumishi wake nao wakijigeuza kuwa watumishi wenye wongofu, lakini mwisho wao utakuwa umepatana na kazi zao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi si jambo la ajabu kama watumishi wake vilevile wanajigeuza kuwa watumishi wa haki. Kwa mwisho wao watalipwa kufuatana na matendo yao.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi si neno kubwa wakhudumu wake nao wakijigeuza wawe mfano wa wakhudumu wa haki. Mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.