2 Corinthians 11:17 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ninachosema sasa si kile alichoniagiza Bwana; kuhusu jambo hili la kujivuna, nasema tu kama mtu mpumbavu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ninayosema kuhusiana na huku kujisifu kwa kujiamini, sisemi vile Bwana Isa angesema, bali kama mjinga.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ninenalo silineni agizo la Bwana, bali kama kwa upumbavu, katika ujasiri huu wa kujisifu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini mimi sizungumzi kwa namna ambavyo Bwana angelizungumza. Mimi ninajivuna kama vile mjinga.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ninachosema sasa si kile alichoniagiza Bwana; kuhusu jambo hili la kujivuna, nasema tu kama mtu mpumbavu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ninachosema sasa si kile alichoniagiza Bwana; kuhusu jambo hili la kujivuna, nasema tu kama mtu mpumbavu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ninayosema kuhusiana na huku kujisifu kwa kujiamini, sisemi kama vile ambavyo Bwana angesema, bali kama mjinga.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ninayosema kuhusiana na huku kujisifu kwa kujiamini, sisemi kama vile ambavyo Bwana Isa angesema, bali kama mjinga.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ninenalo silineni agizo la Bwana, bali kama kwa upumbavu, katika ujasiri huu wa kujisifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ninachosema sasa si kile alichoniagiza Bwana; kuhusu jambo hili la kujivuna, nasema tu kama mtu mpumbavu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ninayoyasema sasa, siyasemi kuwa maneno ya Bwana, ila nayasema kama ya upuzi tu kwa hivyo, tulivyoyafikia majivuno.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ninenalo silineni agizo la Bwana, bali kama kwa upumbavu, katika ujasiri huu wa kujisifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maneno haya ninayosema sasa hayafuatani na mapenzi ya Bwana, lakini ninayasema tu kama mupumbafu kuelekea jambo hili la kujivuna.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nisemalo silisemi agizo la Bwana, bali kama kwa upumbavu, katika ujasiri huu wa kujisifu.