2 Corinthians 11:2 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ninawaoneeni wivu lakini ni wivu wa Mungu; maana nyinyi ni kama bikira safi niliyemposa kwa mwanamume mmoja tu ambaye ndiye Kristo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ninawaonea wivu, wivu wa kiungu, kwa kuwa mimi niliwaposea mume mmoja, ili niwalete kwa Al-Masihi kama mabikira safi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nina wivu unaotoka kwa Mungu kwa ajili yenu. Niliahidi kuwatoa ninyi kama bibi harusi kwa mume mmoja. Niliahidi kuwatoa ninyi kwa Kristo muwe bibi harusi wake aliye safi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ninawaoneeni wivu lakini ni wivu wa Mungu; maana ninyi ni kama bikira safi niliyemposa kwa mwanamume mmoja tu ambaye ndiye Kristo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ninawaoneeni wivu lakini ni wivu wa Mungu; maana nyinyi ni kama bikira safi niliyemposa kwa mwanamume mmoja tu ambaye ndiye Kristo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ninawaonea wivu, wivu wa Kimungu, kwa kuwa mimi niliwaposea mume mmoja, ili niwalete kwa Kristo kama mabikira safi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ninawaonea wivu, wivu wa Kimungu, kwa kuwa mimi niliwaposea mume mmoja, ili niwalete kwa Al-Masihi kama mabikira safi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa niliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ninawaoneeni wivu lakini ni wivu wa Mungu; maana nyinyi ni kama bikira safi niliyemposa kwa mwanamume mmoja tu ambaye ndiye Kristo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani wivu, ninaouona kwa ajili yenu, ni wa Kimungu; maana naliwaposea ninyi mume mmoja, ni Kristo, niwapeleke kwake kuwa mwanamwali mwenye kutakata.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi ninasikia wivu kwa ajili yenu sawa vile Mungu anavyousikia vilevile. Kwa maana ninyi ni kama binti mukamilifu niliyemwowesha kwa mume mumoja, ndiye Kristo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; maana naliwaposea mume mmoja, nimletee Kristo bikira safi.