2 Corinthians 11:20 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mnamvumilia hata mtu anayewafanya nyinyi watumwa, mtu mwenye kuwanyonya, mwenye kuwakandamiza, mwenye kuwadharau na kuwapiga usoni!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kweli ni kwamba mnachukuliana na mtu akiwatia utumwani au akiwatumia kwa ajili ya kupata faida, au akiwanyang’anya, au akijitukuza mwenyewe, au akiwadanganya.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana mwachukuliana na mtu akiwatia utumwani, akiwameza, akiwateka nyara, akijikuza, akiwapiga usoni.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nasema haya kwa sababu mnamvumilia hata mtu yule anayewatumia vibaya. Mnawavumilia wale wanaowarubuni akili na kudhani kuwa wao ni bora kuliko ninyi, au wanaowapiga usoni!
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mnamvumilia hata mtu anayewafanya ninyi watumwa, mtu mwenye kuwanyonya, mwenye kuwakandamiza, mwenye kuwadharau na kuwapiga usoni!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mnamvumilia hata mtu anayewafanya nyinyi watumwa, mtu mwenye kuwanyonya, mwenye kuwakandamiza, mwenye kuwadharau na kuwapiga usoni!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kweli ni kwamba mnachukuliana na mtu akiwatia utumwani au akiwatumia kwa ajili ya kupata faida au akiwanyang'anya au akijitukuza mwenyewe au akiwadanganya.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kweli ni kwamba mnachukuliana na mtu akiwatia utumwani au akiwatumia kwa ajili ya kupata faida au akiwanyang’anya au akijitukuza mwenyewe au akiwadanganya.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana mwachukuliana na mtu akiwatia utumwani, akiwameza, akiwateka nyara, akijikuza, akiwapiga usoni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mnamvumilia hata mtu anayewafanya nyinyi watumwa, mtu mwenye kuwanyonya, mwenye kuwakandamiza, mwenye kuwadharau na kuwapiga usoni!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwavumilia, mtu akiwafanya watumwa, akiwala, akiyatwaa yaliyo yenu, akijikuza, akiwapiga usoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana mwachukuliana na mtu akiwatia utumwani, akiwameza, akiwateka nyara, akijikuza, akiwapiga usoni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Munavumilia hata mutu anayewatia katika utumwa, anayeiba mali zenu, anayewagandamiza, anayewazarau na anayewapiga kofi kwenye uso.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana mwavumilia na mtu akiwatieni utumwani, akiwameza, akiwateka, akijikuza, akiwapiga usoni.