2 Corinthians 11:21 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa aibu nakubali kwamba sisi tulikuwa dhaifu. Iwe iwavyo, lakini kama kuna mtu yeyote anayethubutu kujivunia kitu — nasema kama mtu mpumbavu — mimi nathubutu pia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa aibu inanipasa niseme kwamba sisi tulikuwa dhaifu sana kwa jambo hilo! Lakini jambo lolote ambalo mtu mwingine angethubutu kujisifia, ninene kama mjinga, nami nathubutu kujisifu kuhusu hilo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nanena kwa jinsi ya kujidhili kana kwamba sisi tulikuwa dhaifu. Walakini, akiwa mtu anao ujasiri kwa lo lote, (nanena kipuuzi), mimi nami ninao ujasiri.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninaona aibu kusema haya, lakini tulikuwa “dhaifu sana” kuyafanya mambo kama hayo kwenu. Lakini kama kuna mtu aliye jasiri vya kutosha kujivuna, nami nitajivuna pia. (Ninaongea hivi kama mjinga.)
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa aibu nakubali kwamba sisi tulikuwa dhaifu. Iwe iwavyo, lakini kama kuna mtu yeyote anayethubutu kujivunia kitu—nasema kama mtu mpumbavu—mimi nathubutu pia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa aibu nakubali kwamba sisi tulikuwa dhaifu. Iwe iwavyo, lakini kama kuna mtu yeyote anayethubutu kujivunia kitu — nasema kama mtu mpumbavu — mimi nathubutu pia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa aibu inanipasa niseme kwamba sisi tulikuwa dhaifu sana kwa jambo hilo! Lakini cho chote ambacho mtu mwingine ye yote angethubutu kujisifia, nanena kama mjinga, nami nathubutu kujisifu juu ya hilo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa aibu inanipasa niseme kwamba sisi tulikuwa dhaifu sana kwa jambo hilo! Lakini chochote ambacho mtu mwingine yeyote angethubutu kujisifia, nanena kama mjinga, nami nathubutu kujisifu juu ya hilo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nanena kwa jinsi ya kujidhili kana kwamba sisi tulikuwa dhaifu. Lakini, ikiwa mtu anao ujasiri kwa lolote, (nanena kipuuzi), mimi nami ninao ujasiri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa aibu nakubali kwamba sisi tulikuwa dhaifu. Iwe iwavyo, lakini kama kuna mtu yeyote anayethubutu kujivunia kitu – nasema kama mtu mpumbavu – mimi nathubutu pia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naona soni nikisema: Hayo hatuyawezi, tu wanyonge; lakini jambo lo lote, mtu alilojipa moyo wa kujivunia, (nasema kipuzi) nami najivunia lilo hilo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nanena kwa jinsi ya kujidhili kana kwamba sisi tulikuwa dhaifu. Walakini, akiwa mtu anao ujasiri kwa lo lote, (nanena kipuuzi), mimi nami ninao ujasiri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninasikia haya ya kuisema: tumekuwa zaifu kwa kufanya vile! Lakini kama watu wengine wanasubutu kujivuna juu ya kitu chochote, mimi vilevile nitajivuna. Sasa ninasema kama vile mupumbafu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nanena kwa jinsi ya kujidhili kana kwamba sisi tulikuwa dhaifu. Illakini, akiwa mtu anao ujasiri kwa lo lote, (nanena kipuuzi), na mimi niuao ujasiri.